Ghaddaffi alimsaidia Idd Amin kuvamia Tanzania...

Ha ha ha! hilo hawataki kulisikia kabisa! na uwaulize kosa la Idd Amin ni lipi? hawana jibu muafaka!

duu elimu ya madrasa inakula ubongo wenu kabisa ndugu zangu,. Yani mnawaza udiniudini tuu
 

Watu wote waliomsifia na kumlilia Gadaffi walitumia jicho la DINI kwakuwa ni mwenzetu hata kama aliwaua Watanzania wenzetu bila SABABU ili amsaidie Amin ambaye naye alikuwa mtu wa DINI yake.
 

Katika Mafundisho ya BIBLIA tumeambiwa/amriwa kusamehe na kuwapenda maadui zetu kwa hiyo wale waliomkumbatia huenda walimsamehe wao kama wao na kumpenda.
 
Mbona wazungu tunawakumbatia wakati walinyanyasa babu zetu?
 
me binafsi alipouwawa Gadaff nkashindwa hata kula nliuzunika sana......labla nikupe kwanini watanzania wamemlilia Gadaff na kumkumbatia sababu Watanzania hasa wabara ni watu wasamehevu wenye kusahau yaliyopita lakini kama aliyoyafanya Gadaff angeyafanya zanzibar basi mpaka leo angelaaniwa maana hawa ndugu zetu wabora wa kulaani kama mungu wao peke yao....Tz ilishayasamehe yalyopta na tumemlilia Gadaff na tutamkumbuka kwa msimamo wake katka bara la Africa.......
 
Huyu Gagafi aliuwa waislamu wenzetu wengi sana pale Bukoba mjini!
 
..Iddi Amin alikuwa anaua hata Waislamu wenzake.

..tafuteni historia ya Shaban Kirunda Nkutu aliyepata kuwa Waziri wa Afya wa Uganda.
 
😱hwell:
 
..Iddi Amin alikuwa anaua hata Waislamu wenzake.

..tafuteni historia ya Shaban Kirunda Nkutu aliyepata kuwa Waziri wa Afya wa Uganda.
Mkuu umeenda mbali sana, ni rais wa siku 3 wa Uganda ambaye hakutangazwa, na hiyo ni kwa sheria za jeshi pamoja na zile za UN, Brig Gen (RTD)Benjamin Msuya, hakuna asichojua kuhusu mauaji ya hao ndugu.
 
Thanda,

..hahahaa!!

..habari za Maj.Gen.Ben Msuya kuhusu Uganda umezipata wapi??

..mimi nilizisoma kwenye kitabu kilichoandikwa na waandishi wa habari wa Uingereza.

..ni kweli Ben Msuya[then Lt.Col] alikuwa incharge wa utawala Kampala wakati Amini amekimbia na Prof.Yusuf Kironde Lule hajaapishwa.

..kwa kweli kuna ulazima wa kuandika historia ya vita vya Kagera, na kuanzisha makumbusho ya vita vya Kagera.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Joka Kuu, nilibahatika kukutana na Benjamin Msuya, siku moja baada ya kuwa na Chacha D. Igoti, na ndipo alipotueleza historia ndeefu ya maisha yake, hiyo ni pamoja na kutupatia some important documents ambazo hadi leo nimezitunza. Ukaribu wangu ulikuja kutokana na mimi kuoa mkurya wa tofauti kitabia na msomi mwelimika(kwa sasa tuko naye hapa Dar.) Sasa huyu binti baba yake na Igoti ni marafiki wa muda mrefu sana hivyo kulazimika kutukutanisha..ni story ndefu kidogo na muda umepita tangu nionane na Benjamin Msuya, ila naamini yupo hapa Dar. Ngoja nitamwuliza baba mkwe kujua anaishi wapi nione kama nitaweza kumwona kabla sijaondoka....Mkuu JF ni Chuo...kinafundisha mengi na kuwakutanisha wengi humu.
 
Thanda,

..ukikutana Maj.Gen.Msuya tena mshauri yeye na wenzake wa generation iliyopigana vita vya Msumbiji,Seychelles,Comoro,na Uganda, etc waandike historia yao.

..hebu fikiria tukio la dakika 30 za kumuua Osama Bin Laden wameshatengeza documentaries na kuandika vitabu, kwanini na sisi wa-Tanzania tuliopigana vita ya miezi 9 hatuweki kumbukumbu zetu??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakuhakikishia nitafanya hivyo, ukweli ni kwamba aliyeleta hii thread amenikumbusha mtu ambaye yuko hapahapa Dar halafu nisimuone. hii ingekuwa ajabu na kweli kama sio uongo.Asante Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…