Ghana: Mishahara ya Mawaziri na Rais yapunguzwa kwa 30%

Ghana: Mishahara ya Mawaziri na Rais yapunguzwa kwa 30%

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Ghana Nana-Akufo Addo na mawaziri wake wamepunguza mishahara yao kwa kiwango cha asilimia 30 kama hatua za kupunguza matumizi ya serikali, wakati nchi inakabiliwa na gharama kubwa za mafuta kutokana na mzozo wa Ukraine na kukwama kwa mswada wa sheria kuhusu kodi mpya.

Waziri wa fedha Ken Ofori-Atta ametangaza marufuku ya safari za nje kwa maafisa wa serikali, isipokuwa zile zenye umuhimu mkubwa, na ununuzi wa magari yanayoagizwa nje umesitishwa mara moja.

Amesema serikali inatarajia kuokoa karibu dola milioni 400 kupitia hatua hizo.

Bei ya mafuta ulimwenguni imeongezeka kwa viwango vya juu sana kwa sababu ya vita kati ya Russia na Ukraine, na kusababisha ongezeko la gharama ya maisha na usafiri kwa namna ambayo imeathiri sana nchi za Afrika magharibi kama Ghana.

Serikali ya Ghana inasumbuka pia kuongeza kodi ya mapato ya ndani wakati bunge limeshindwa tangu mwaka jana kupitisha mswada wa sheria wenye utata, wa kuongeza kodi ya asilimia 1.75 kwa lengo la kuongeza mapato ya serikali.

“Ni muhimu kusisitiza wazi kwamba, matatizo tunayokabiliana nayo nchini Ghana si ya Ghana pekee”, taarifa ya waziri wa fedha imesema.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “Serikali katika nchi tajiri na nchi maskini zote zinashughulika na kuja na maagizo ya kufufua tena uchumi wao, baada ya athari mbaya za Covid 19 ambazo zilidumaza usambazaji wa bidhaa kote ulimwenguni, bila kusahau vita vinavyoendelea kati ya Russia na Ukraine.”

Hatua nyingine ni kupunguza kwa asilimia 50 ruzuku ya mafuta iliyokuwa inapewa wateule wa kisiasa na wakuu wa taasisi za serikali.

VOA
 
Hilo la kubana matumizi alilifanya mwenda zake lakini mishahara yao hakuigusa alafu tukaendelea kumshangilia na kumpigia makofi
 
Mkuu bado unaomboleza pole sana. Kabla akina mbowe hawajafyekwa bungeni suala hilo lilishajadiliwa na wabunge wote(upinzani na ccm) wakaungana kupinga maslah yao kuguswa
Hilo la kubana matumizi alilifanya mwenda zake lakini mishahara yao hakuigusa alafu tukaendelea kumshangilia na kumpigia makofi
 
Mama Samia akileta huo mchezo hapa bongo soon watamu RIP😅
Tanzania unaweza kukuta tatizo siyo ukubwa wa mishahara.

Tatizo kubwa Ni "Mlundikano was posho na marupurupu" nje ya mishahara ambazo kwasababu siyo mishahara haziwi subjected to Taxes.

Mfano: Mbunge mshahara wake wa kwenye salary slip Ni Tsh 3.8M.

Mshahara wa Rais kwenye salary slip Ni Tsh 16M.
 
Huku Tanzakiza pesa za tozo zinakwenda kumlipa zit* na Prof mkind* na kamati za tume huru air
 
Hawa nao ni vibaraka tu, wapigane hukooooo ukaraine njaa upate wewe mwafrika?
Miaka yote wazungu wanaua watu na kupigana hapo kwa waarabu mbona hakuna njaa iliyoingia afrika?
Propaganda tu na uvivu wa kulima wa hao ghana,
Viongozi wa hivi wanatumika sana
Putin kazia hapohapo
 
Back
Top Bottom