Ghandhi na mtazamo chanya

Ghandhi na mtazamo chanya

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
MOHANDAS KARAMCHAND MAHATMA GANDHI BABA WA TAIFA LA INDIA AMBAYE ALIKUWA NI KIONGOZI WA DINI YA KIHINDU, MWANAHARAKATI NA MKOMBOZI ALIYEFANIKIWA KULIPATIA TAIFA LAKE UHURU.



Na, Comred Mbwana Allyamtu.
MONDAY 11/9/2017.


Mohandas Karamchand Gandhi alizaliwa tarehe 2 Oktoba 1869 na kufariki dunia tarehe 30 Januari 1948, pia ni maarufu zaidi kwa jina la Mahatma Gandhi, alikuwa mwanasheria, mwanafalsafa, mpiganaji wa haki za binadamu na kiongozi dini na pia alikuwa ni kiongozi wa siasa nchini India. Anajulikana hasa kama kiongozi wa harakati za uhuru wa India aliyepinga ukoloni na kushinda ukoloni kwa njia ya amani bila ya matumizi ya mabavu au silaha.

Gandhi alizaliwa katika eneo la mji wa Gujarat kama mtoto wa mzee Karamchand Gandhi na mama yake alijulikana kama Putali Bai. Baba yake alikuwa waziri mkuu katika serikali ya jimbo la Maharaja wa nchi ndogo ya Porbandar wakati huo jimbo hilo ilipokuwa sehemu ya India ya Kiingereza. Familia yake ilifuata dini ya Uhindu madhehebu ya Wavishnu lakini nyumba ya baba yake na Gandhi ilitembelewa pia na Waislamu na Wajain. Mwaka 1883 akiwa na umri wa miaka 13 aliozwa kwa mke wake Kasturba wakazaa watoto 4.

GHANDI APELEKWA UINGELEZA MASOMONI.

Mwaka 1888 alisafiri kwenda Uingereza ambapo aliamu kusoma sheria kwenye chuo kikuu cha London, ambapo baada ya kuhitimu akapokewa kama wakili kwenye mahakama za juu kuanzia 1891 alipokuwa huko uingeleza. Huko Uingereza alisoma mengi juu ya dini ya Ukristo, akipendezwa hasa na mahubiri ya Yesu na hotuba ya mlimani, lakini hakuvutwa na nafasi ya pekee Yesu anayopewa katika imani ya Kikristo. Wakati uleule alianza kusoma vitabu vitakatifu vya Uhindu, hasa “Bhagavad Gita” iliyoendelea kuwa mwongozo wa kiroho maishani mwake.


MAISHA YA MAHATMA GHANDI NCHINI AFRIKA YA KUSINI

Baada ya kuhitimu chuo baadae aliamua alirudi india akafanya kazi kama wakili mjini Bombay. Mwaka 1893 alitumwa Afrika Kusini Kwa kesi moja tu, lakini alibaki huko hadi 1914. Katika Afrika Kusini Gandhi alijenga falsafa yake, akaanza kujishughulisha na masuala ya siasa na haki za binadamu. Alihamasishwa kufanya hivyo kutokana na sera ya ubaguzi wa rangi iliyokuwa nchi humo. Gandhi alisimulia katika kitabu chake kimoja juu ya maisha yake ya kwamba siku chache baada ya kufika Afrika Kusini alisafiri kwa treni akishika tiketi ya daraja la kwanza. Abiria Wazungu walilalamika juu yake akaambiwa ahamie kwenye behewa la mizigo. Gandhi alikataa akaondolewa na polisi akabaki kituoni.

Baadaye alipata Mang'amuzi mengine alipofukuzwa katika basi Kwa sababu Mzungu aliyeingia alidai kiti kilichokaliwa na Gandhi. Hivyo Gandhi alifungua ofisi katika Afrika Kusini mjini Durban kwenye jimbo la Natal akaanza kupigania haki ya Wahindi katika Afrika Kusini waliobaguliwa kwa sheria za nchi hiyo. Wakati ule Wahindi walikuwa raia wa Milki ya Kiingereza wenye haki zote wakifika Uingereza penyewe, lakini katika Afrika Kusini iliyokuwa pia sehemu ya milki ya Kiingereza walibaguliwa kutokana na rangi ya ngozi yao. Mwaka 1894 aliunda chama cha Natal Indian Congress (NIC)akifuata mfano wa Indian National Congress huko India. Chama hicho kilidai haki sawa Kwa Wahindi katika Afrika Kusini. Ghandi Wakati wa Vita ya pili ya Waingereza dhidi ya Makaburu (1899) na vita dhidi ya Wazulu (1906) aliunda kikosi cha usaidizi kwa Waingereza waliokusanya majeruhi na kuwatunza kwenye hospitali. Mwaka 1906 serikali ya jimbo la Transvaal ilianzisha sheria iliyodai Wahindi kujiandikisha na kubeba vitambulisho. Gandhi alipinga sheria hiyo akaongoza maandamano na mikutano ya kuchoma vitambulisho. Alihimiza wafuasi wake kukubali kupigwa na kuadhibiwa bila ya kutumia mabavu wenyewe.

Katika miaka iliyofuata Wahindi maelfu walipigwa na polisi, walikamatwa na kufungwa jela pamoja na Gandhi mwenyewe. Baada ya miaka saba watu wengi walisikitikia matumizi ya nguvu dhidi ya Wahindi walioandamana kitulivu, hata serikali ilipaswa kupunguza ukali wa sheria.

FALSAA YAKE ALIYOANZISHA YA ‘’Satyagraha’’
Katika miaka híyo Gandhi alijenga falsafa yake ya upinzani bila ya silaha wala mabavu aliyotumia baadaye India. Imani ya Gandhi iliathiriwa na mafundisho ya dini ya Ujain aliyojua tangu utoto wake na hasa dai la “kutotumia mabavu lakini kufuata njia za amani’’. Kiini chake kilikuwa satyagraha inayomaanisha "kusimama upande wa ukweli". Satyagraha kwake ilikuja pamoja na kutokuwa na uhasama na kutotumia nguvu. Alisema "Ukweli haukubali nguvu Kwa sababu hakuna mtu mwenye ukweli wote, kwa hiyo hakuna mwenye haki ya kuadhibu wengine." Dhana nyingine aliyoanzisha ni "swaraj" inayomaanisha "kujitawala".

Gandhi aliona swaraj Kwa ngazi mbili: kwanza swaraj kama kujitawala kwa kila mtu akitawala tamaa zake; alafu pili swaraj kama haki ya watu kwa pamoja kujiamulia mambo yao na kutotawaliwa na watu wa nje (kwa mfano na wakoloni).

MAHATMA GHANDHI ALEJEA INDIA MWAKA 1914

Baada ya kuugua aliondoka Afrika Kusini 1914 akarudi Uhindi alipopokewa kama shujaa kwa sababu habari zake zilimtangulia. Kutokana na kuonekana kama mtetezi wa wahindi alipokuwa nchini afrka kusini. Aliunda makazi ya pamoja yaliyofahamika kama (ashram) alimoishi pamoja na watu waliofuata imani yake ya satyagraha. Alianza kuvaa nguo za wakulima wa kawaida. Hatmae Mwaka 1920 alikuwa kiongozi wa chama cha ukombozi cha india (INC) Indian National Congress akaanzisha kampeni ya kitaifa dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza. Alihimiza Wahindi wengi kutotii sheria za serikali ya Kiingereza bila kutumia nguvu.

Mfano moja ni maandamano ya chumvi (Salt Demonstration) mwaka 1930. Sheria ya Kiingereza iliweka biashara yote ya chumvi mikononi mwa serikali. Kutengeneza chumvi na kuiuza ilikuwa haki ya serikali iliyokabidhi haki hii kwa makampuni waliolipa kodi za pekee. Gandhi aliongoza watu maelfu baharini walipochota maji ya bahari wakaichemsha na kupata chumvi kidogo kwa njia hiyo. Kiasi cha chumvi kilikuwa kidogo mno, lakini kwa kufanya hivyo walivunja sheria kwa kusudi. Waingereza walianza kuwakamata wapikachumvi, lakini walishindwa na idadi kubwa ya watu waliokubali kukamatwa. Tena ilikuwa vigumu kuwahamasisha askari walioona kosa lilikuwa dogo sana na wakosaji hawakuwa hatari yoyote kwao.

Gandhi mwenyewe alikamatwa mara kadhaa akakaa jela jumla ya miaka 8. Mwishowe watu wengi huko Uingereza walichoka habari za vuguvugu la kudai uhuru wa India na mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia serikali mpya ya chama cha Labour ya huko uingeleza iliamua kuipa India uhuru wake.

KUGAWANYIKA KWA INDIA NA PAKISTANI NA MSIMAMO WA MAHATMA GHANDHI

Ndani ya India wenyewe fitina ilianza juu ya nafasi ya Waislamu katika taifa jipya, huku sehemu kubwa ya Waislamu wakidai kugawiwa nchi yao kwa koloni katika nchi mbili. Mapigano yalianza na watu maelfu waliuawa. Mnamo Agosti 1947 nchi mbili za india na Pakistan zilianzishwa, na Oktoba 1947 vita vikafuata kati ya nchi zote mbili juu ya jimbo la Kashmir. Vita vikaongeza uadui, na watu mamilioni walifukuzwa yaani Wahindu kutoka Pakistan na Waislamu kutoka Uhindi. Gandhi alijitahidi kupatanisha viongozi wa pande zote bila mafanikio binasfi alichukizwa na kugawanyika kwa nchi yao ya Uhindi na kuwa mataifa mawili mara kadhaa Ghandhi aliwalaumu wanasiasa kusababisha migogolo hiyo kimsingi Ghandhi akafunga kula chakula kama mashaliti ya kutaka kumalizwe mgogolo huo akitangaza alikuwa tayari kufunga hadi kifo wasipopatana. Kwa Heshima ya Gandhi kwa viongozi wa dola hilo ilisababisha viongozi wa pande mbalimbali katika India kukutana na kutafuta njia za kumaliza uhasama huo jambo liloanza kuleta unafuu wa machafuko hayo.

KIFO CHAKE CHA KUUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MWAKA 1948

Ilikuwa ni Tarehe 30 Januari 1948 Gandhi alipigwa risasi na kuuawa alipo kuwa akitembea katika bustani ya nyumba yake huko New Delhi. Mwuaji wake alikuwa Mhindu wa kundi lililofuata itikadi kali. Huyu kijana alikasirishwa sana na hatua za kupatanisha Waislamu na Wahindu akaamini kuwa Gandhi alikuwa msaliti wa dini ya Uhindu.

Mahatma Gandhi alijulikana hasa kwa jina la Mahatma. Neno hili lilitokana na lugha ya Kisanskrit linalo maanisha "roho kubwa". Aliitwa hivyo mara ya kwanza alipofika Bombay wakati wa kurudi kutoka Afrika Kusini. Gandhi hakupenda jina hilo lakini alishindwa kuzuia matumizi yake.
e5bffe4c3e7d938d8c246fd662496d5d.jpg
66bcb572a1c1cacf64c04b5675ec1dfb.jpg

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom