KERO Gharama kubwa za kufanya maombi ya kazi kwa baadhi ya Taasisi za Serikali

KERO Gharama kubwa za kufanya maombi ya kazi kwa baadhi ya Taasisi za Serikali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kama kichwa cha habari hapo juu. Baadhi ya taasisi za serikali kama TAA, TANROADS nk zimekuwa zikitoa mahanadi za kazi na kuwataka waombaji waombe kwa mfumo wa Posta tu, lakini pia hutakiwa kucertify vyeti.

Gharama ni kama zifuatazo;
1. Photocopy ni zaidi ya elfu 2 mpaka 3
2. Kucertify vyeti inategemea na jumla ya vyeti ila si chini ya elfu10
3. Posta kwa EMS 15000
4. Gharama za usafiri kwa sisi tunaotoka vijijini 12000.

Hivi kweli dunia ya leo kuna ulazima gani wa kuwalazimisha watu watume maombi kwa njia ya posta tu ambayo ni analogue. Watu wengi wanashindwa kuomba kwa sababu ya gharama kubwa na wakati mwingne unaweza kuomba na usipate hiyo nafasi yenyewe.

Dunia imehamia kiganjani,watu wanapaswa kufanya maombi kupitia hata kwenye simu through emails na kama haiwezekani sana bora mkazipeleka Ajira portal

Screenshot_20241207_121424_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom