SoC01 Gharama kubwa za matibabu zinafanya watu kuishi na ulemavu

SoC01 Gharama kubwa za matibabu zinafanya watu kuishi na ulemavu

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Hii imenigusa niliongelee hili ampapo Kutoka mkoani Mbeya yupo kijana aitwaye Jackson ni kijana ambaye alizaliwa akiwa na matatizo mbalimbali hata hivyo kijana huyo anaeishi na wazazi wake akiwa ni baba mzazi na mama mlezi ambapo pamekuwa na changamoto ya mtoto huyo kushindwa kwenda shuleni kutokana na hali yake tete ya ulemavu ambapo kwanza kabisa hana vifaa vya vitakavyowezesha yeye aweze kwenda shuleni mfano mzuri baskeli za walemavu hata hivyo mara kadhaa wazazi wake wamejitahidi kujichanga na kwamba angalau waweze kumtibia hali yake lakini jambo limekuwa kazi bure.

Kijana huyo aitwaye (Jackson) jina ambalo ni Mbadala wa jina lake mwenye angalau miaka 13. Amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo uitwao (spinal bifida) ni ugonjwa ambao umemfanya ashindwe kutembelea miguu badala yake amekuwa ni mtu anayekaa tu mahala pamoja na pia ni ugonjwa ambao umemfanya hawezi kuhisi haja zote hivyo ni kutokana na baadhi ya mifumo ya fahamu kutokukaa vizuri kutokana na tatizo hilo la uti wa mgongo.

Anaishi katika hali mbaya sana kwakuwa hata kuna muda mwingine marafiki zake wanamnyanyapaa japokuwa muonekano wa afya yake ni njema kabisa. Sasa linapokuja swala la matibabu wazazi wake vichwa vinawauma na ni hali ambayo inamdhoofisha kiujumla, Wamejaribu kwenda mara kadhaa kwenye hospitali kubwa ikiwemo muhimbili ili wapate tiba lakini imeshindikana kutokana na kutokuwa na kiwango stahiki cha fedha chenye kukidhi gharama za matibabu hayo.

Hivyo ningeliomba Serikali iweze kupunguza gharama za matibabu kwa wazee na watoto ili kuweza kuimarisha afya za walengwa hao... Kwakuwa hatuwezi jua kwamba huyo mtoto angelipata matibabu tangu anazaliwa labda leo angefika mbali, na hata baadae angelikuja kuwa mtu mkubwa kwa kuwa Siku zote mungu hubariki pale pasipodhaniwa


Tunapoomba Mungu atubariki hutubarikia lakini kwa macho ya nyama hatuoni baraka zake hutupatia baraka kwa namna ambazo kamwe hatuwezi kujua kwamba ndo baraka zenyewe na hatimaye mtu akiona mungu kampatia mtoto mlemavu au mwenye kasoro anaanza kumlaani mungu na kuona kama huyo mtoto ni mzigo kwake lakini huwa hatufikirii kwa upande wa pili kwamba je? Mungu anamakusudi gani kunipa huyu mtoto, yaweza kua ulikua hujui kwamba sawa umehangaika lakini mlemavu huyo ambaye ulimchukia huenda ndiye atakaechangia maisha yako kuwa mazuri na kubadilika kabisa siku za usoni

Kwa hiyo ni ombi langu la dhati kwamba tuwapende walemavu, tuwatunze pia tuwajali na kamwe tusiwanyanyapae tuwasikilize na tuwasaidie maombi yao kwa kuwa mungu hakukupa uzima ulionao ili uwe kikwazo kwa walemavu au kwa watu wengine.

Pia naiomba Serikali ijaribu kupunguza gharama za matibabu ili kila mmoja anufaike na huduma za kiafya zinazotolewa na nchi yake ili kwamba aweze kua na afya njema na kusaidia katika ujenzi wa taifa lake. Kwakuwa endapo taifa litakua na wananchi walio na afya njema ni kwamba tutaweza kupigana na umasikini kutokana na shughuli mbalimbali tuzifanyazo.

Asante
Mchana mwema.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom