Unachukua car sale agreement, pamoja na card ya previous owner na TIN yako, unaenda navyo ofisi za TRA (zinazodili na kusajili magari) kuna form watakupatia unaijaza kisha watakufanyia calculation ulipie kiasi gani, kisha watakupatia form ya bank ambapo utapaswa kwenda kulipa hiyo hela, ukishalipia watakutengenezea kadi mpya kulingana na details utakazokuwa umejaza kwenye form ya mwanzo. Ni process ya dakika chache kutegemeana na speed yako. ila andaa kama 200,000 Tsh manake binafsi sikuelewa formula wanayotumia, niliwahi kusajili corolla wakanilipisha 160,000! Labda wajuzi watatufungua macho namna wanavyo calculate gharama...