Responded Gharama vifaa vya ujenzi, tishio kupanda kodi za nyumba

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Ndoto ya Watanzania kumiliki nyumba imeendelea kukumbwa na changamoto kutokana na kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi, hali inayotajwa kuongeza uwezekano wa kupanda kwa kodi za nyumba, kusimama kwa baadhi ya miradi ya ujenzi na kupungua kwa fursa za vibarua nchini.

Ongezeko hilo linahusishwa zaidi na kupanda kwa bei ya mafuta katika miezi ya hivi karibuni, hali iliyoongeza gharama za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa vifaa muhimu vya ujenzi katika maeneo mbalimbali nchini.

Soma zaidi:Makosa 8 ya ujenzi yanayoongeza gharama,epuka kabla haujajuta

Wataalamu wa uchumi na ujenzi wanaonya kuwa, iwapo hali ya kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi itaendelea, athari zake hazitaishia kwa wanaojenga pekee, bali zitawaathiri pia wapangaji, wafanyabiashara na ajira zinazotegemea sekta ya ujenzi.

Akizungumza na Mwananchi jana, Jumapili, Agosti 9, 2026, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Khadija Ngasongo, amesema suala hilo linaangaliwa kwa kina na kwamba Serikali itatoa ufafanuzi wake siku za karibuni.

“Tuachieni, tunaliangalia siku mbili au tatu zijazo Waziri (wa Viwanda na Biashara-Judith Kapinga) mwenyewe atalitolea ufafanuzi wa kina na atawaita waandishi wa habari,” amesema.


Source:Mwananchi

Pia soma: Judith Kapinga: Serikali inafanyia kazi kupanda kwa bei ya sariji ili wananchi wa kawaida waweze kumudu
 
 

Attachments

  • 1000020485.jpg
    12.1 KB · Views: 11
  • E2J15v45XLSQdTMG.jpeg
    58 KB · Views: 11
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…