Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Katika muendelezo wa Makala zangu za Nishati safi ya kupikia; kumekuwa na sintofahamu kuhusu gharama za umeme kwamba ni kubwa sana hivyo kwa kumuwezesha mwananchi ni bora kumpa gesi. Nimeona bora tuangalie ukweli huo kwa kutumia mahesabu yasiyo rasmi....
UFANISI WA VYOMBO VYA UMEME
Kwa sasa kuna vyombo vyenye ufanisi wa kutosha kuliko majiko ya umeme ya zamani ya Coils; Kuna vyombo vina ufanisi zaidi ya mara tatu ya mtu anayepikia gesi (kutokana na upotevu wa Nishati); Kuna Slow Cooker za mpaka Watts 100 (Hii ni sawa sawa na taa za zamani za nje ambazo watu walikuwa wanatumia) yaani ni kama kusema kipindi kile unawasha taa ya nje usiku kucha hapo ungeweza kupika mlo wako wa siku.
KUNA UWEZEKANO WA TANESCO KUSHUSHA UNITS
Tukumbuke ya kwamba mara baada ya kumaliza Bwawa la Nyerere kutakuwa na Ongezeko la Uzalishaji wa zaidi ya mara mbili na gharama za uzalishaji huu ni ndogo kuliko ambavyo tulikuwa tunanunua umeme kwa madalali hivyo kuna uwezekano wa kuwawezesha wananchi wakanunua Units kwa chini ya Tshs 100/= na hata kama wasiposhusha kumbuka kwa sasa kutokana na mahesabu mtu wa kijijini au Tariff Zero ni kama ananunua gesi ya 15kgs kwa elfu Ishirini (kama badala ya kununua gesi angetumia umeme)
TUSIFANYE MAKOSA....; Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanye Tunachoweza
1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 15kgs (ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 15kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 15kgs kuna Units Ngapi
13.6kwh x 15 equals to approx = 204 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 15 una Units takriban 204
BEI ZA UNITS ZA UMEME KWA BEI YA SASA.
Kama tulivyoona Mtungi wa 15Kgs una Units Takriban 204;
Hivyo basi kwa wale wa mijini ambao sasa wananunua Units kwa Tshs. 292/= wakiamua kununua Kwa Pesa ambayo wananunua watu wa gesi itawagharimu
292/= x Units 204 itakuwa sawa na 59,668/=
Kwa Wale wa Vijijini na wa Tariff 0 ambao Units ni Tshs 100 wakiamua kupikia Umeme badala ya Kununua Mtungi wa Gesi
100/= x 204 Units itakuwa sawa na 20,400/=
Hivyo basi kwa dakika hii Bado Umeme ni Bei rahisi na kwa kumwabia mtu anunue gesi kwamba ndio Nishati ya Gharama Nafuu tunapotoka...Kwenye Mtungi wa 15kgs (ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 15kgs kutokana na uzito wa Mtungi)