Gharama ya kujenga huu mjengo

UGOKO MKAVU

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2013
Posts
202
Reaction score
78
Iwe na vyumba vitatu vya kulala na kimoja wapo kiwe ni masterbedroom, jiko + stoo, living & dinning room na choo/bafu la public.

Naomba msaada wa kuchanganua gharama ya kuijenga nyumba kama hii...

Angalizo: kiwanja ninacho
 
Attachments

  • ny.jpg
    28.8 KB · Views: 1,601

Ramani unayo au umepiga picha jengo la mtu?Cha kwanza tafuta ramani mambo mengine baadae...
Ukitaka ramani ni PM tufanye kazi.
 
Ramani unayo au umepiga picha jengo la mtu?Cha kwanza tafuta ramani mambo mengine baadae...
Ukitaka ramani ni PM tufanye kazi.

Ramani yake cna ila nimeikuta sehem nikaipenda. Kikubwa ninachohitaji ni ufafanuzi wa gharama za kuijenga kulingana na mahitaji niliyoyataja hapo awali mkuu...
 
Uko too general hebu fafanua ujenzi/mahitaji na gharama toka msingi mpaka finishing
Swali lako la kwanza limejibiwa kimsingi na mdau ila sasa nadhani unataka jibu la swali lingine.
Kwa kifupi makadirio ya huyu mdau nakubalina anayo kama tu we mwenyewe utakuwepo kusimamia show nzima ya ujenzi from msingi mpaka paa. Hii kitu inawezekana sana na wala haitishi sana.
Ukikomaa nayo kwa style hiyo am sure utapata zaidi ya hiyo nyumba uliyopiga picha hapo juu.
Ni kukomaa na mafundi la sivyo utachunwa kama mbuzi wa vingweta
 
Mkuu hao mbuzi wa vingweta wanachunwaje?

Back to the topic, nitashukuru zaidi ukiweka mchanganuo..
 
Ukipata fundi ambae siyo mwizi na pia kama uwanja wako ni tambarale, hiyo nyumba mpaka finishing vyumba 3 vya kulala na kimoja wapo kiwe ni masterbedroom, jiko + stoo, sitting & dinning room na choo/bafu la public ni M 45 yaani kila kitu kipo tayari mpaka tenki la maji umeweka. Lakini kama nyumba hiyo unaijenga Mbezi ya Kimara andaa si chini ya M65 maana ujenzi wa Mbezi upo juu sana
 
Kiwanja kipo kivule ni tambarare, asante kwa mchango wako
 
Idea nzuri kijana, hayo ndiyo mawazo yakufikiria sasa kwani fainali uzeeni
 
Ramani yake cna ila nimeikuta sehem nikaipenda. Kikubwa ninachohitaji ni ufafanuzi wa gharama za kuijenga kulingana na mahitaji niliyoyataja hapo awali mkuu...
Huwezi kujua gharama za ujenzi bila kuwa na architectural/structural drawings coz kwa kuangalia kwa macho huwezi kujua vipimo sahihi na kisha kuandaa bills of quantity mkuu!!!Ukiwa na full set of working drawings ndio unaweza tafuta gharama za ujenzi kwa project husika..
 
Mkuu hapo kwenye red mbona umenibamba!!!Yaani ni balaa kiongozi,kwanzia kokoto,mchanga,maji,kifusi ni gharama ajabu...
 
Ramani unayo au umepiga picha jengo la mtu?Cha kwanza tafuta ramani mambo mengine baadae...
Ukitaka ramani ni PM tufanye kazi.

Wabongo mijengo ya kuigana hakuna ubunivu wa kubuni kitu chako kipya, hivyo utaona mtaa mzima hadi mji kujaa majengo ya aina hiyo hasa mapaa yake hadi huoni kipya zaidi ya kuga tu.

Kwanza mtindo huu wa paa ni ghali sana ukilinganisha na baadhi ya mapaa ambayo yanaweza kuleta mwonekana mzuri na nyumba ikapendeza ziadi.

Kupendezesha kwa nyumba si mjengo na paa lake tu, ila namna unavyoweza kuintengeneza bustani na miti ya kupamba eneo la nyumba yako kama una kiwanja chenye kuruhusu kufanya hivyo ingawa viwanja vingi vya dar vinaruhusu zaidi nafasi ya nyumba na kutotoa nafasi zaidi kwa bustani, mikoani kumesheheni viwanja vya kuwaga fanya upendavyo ardhi mali ya umma.
 
Kiwanja kipo kivule ni tambarare, asante kwa mchango wako

Huko ni tambarale plus maji na mchanga havina taabu hata kidogo,mkuu wala usihangaike kama ni Kivule mpaka finishing fundi asipokuchakachua hiyo ni 35 millions akikuchakachua ndiyo 40 millions
 
Mkuu hapo kwenye red mbona umenibamba!!!Yaani ni balaa kiongozi,kwanzia kokoto,mchanga,maji,kifusi ni gharama ajabu...

Yaani Mbezi ya Kimara ni issue kwenye mambo ya ujenzi,nyumba ambayo unaijenga Mbezi kwa 40M hiyo hiyo nyumba ukiijenga Mbagala ama huko Mbande unaijenga kwa 30M
 
30m nakubali. Hii nyumba labda ni 12m by 10m. Msingi wake ni less than 7m. Usipige jamvi. Weka kifusi pandisha Kwa 3m. Kisha funika Kwa 7M. Badaa ya hapo finishing 10M.
 
30m nakubali. Hii nyumba labda ni 12m by 10m. Msingi wake ni less than 7m. Usipige jamvi. Weka kifusi pandisha Kwa 3m. Kisha funika Kwa 7M. Badaa ya hapo finishing 10M.
Anayepinga 60 -65 Hajawahifanya hii mambo. Mkuu hilo ni jibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…