Gharama Ya Solar Power

Gharama Ya Solar Power

Ibravo

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
539
Reaction score
202
Habari Wanajamvi.
Naomba kujuzwa juu ya gharama za solar power(Full Gadgets i.e Charger Controller,Panel,Battery & Inverter ) ambayo nitaweza kuwasha Tv,King'amuzi pamoja na Taa Sita.Mwenye Ufahamu Navyo Tafadhari.
 
Mkuu,nimeweka kutumia kampuni ya mionzijua gharama ya bila wiring ni tshs.950,000.ila kama watakufanyia na wiring ni tshs.1.5m kwa kila kitu.
 
Inategemea na aina ya tv, kama ni flat btr 65ah,soj 80w, controler 10amp,inveter 200w.ubora wa vifaa ni muhimu> 600000.
 
Nashukuru sana wadau!!
Ila mimi nina kachumba changu kamoja sasa kwa gharama ya 1.5Mil kwa chumba kimoja ni shida aisee,labda niitafute hiyo 600,000 maana ndio nafuu angalau.
 
kama upo dar au mkoa wa pwani.,andaa 587000 nitafute kupitia namba 0785477684 nitakufungia chin ya usimamizi wa kampuni ya steps solar
 
Mliopo Dar hamuhitaji solar power itakayotosha fridge? Maana sioni imejumuishwa, na ni muhimu iwepo.

Itabidi kuongeza uwezo wa hizo inverter, betri, panels na controler.

Ukiamua kula nguruwe basi ule aliyenona.
 
sola system ya kuendesha fridge,taa 8 pamoja,dek,fen,dicoda,tv pamoja na radio ipo andaa 3.9 ml umeme wa uhakika kwa warant ya miaka 25 chin ya uangalizi wa steps solar
 
Ulieuliza swali la kuongezea Fridge umesaidia wengine hapa.

Halafu naomba wengine mtujuze hii issue ya Tanesco kuingilia mradii huu,nasikia kwamba kuna charges unalipia tanesco kwa kutumia Solar power kila mwezi?hata kama sio dili lao.Mambo ya Serikali hayo.

Mfano ni huku Zanzibar,kwamba ukichimba kisima cha maji basi lazima kila mwezi ulipie Idara ya Maji.Hapo Malipo ni ya kufikrika tu,maana kila mtu analipa bei yake.
 
Malipo ni ya kufikrika tu apo hakuna kitu kama icho cha kulipia tanesco au idara za maji,
 
sola system ya kuendesha fridge,taa 8 pamoja,dek,fen,dicoda,tv pamoja na radio ipo andaa 3.9 ml umeme wa uhakika kwa warant ya miaka 25 chin ya uangalizi wa steps solar
Mkuu hivi vifaa nikiviwasha fully kwa pamoja, hio solar power inaweza kuhimili kwa muda wa masaa mangapi kabla umeme kwenye inverter haujaisha??
 
Mkuu hivi vifaa nikiviwasha fully kwa pamoja, hio solar power inaweza kuhimili kwa muda wa masaa mangapi kabla umeme kwenye inverter haujaisha??

nikusahihishe kwanza, umeme hutunzwa kwenye betri sio invetor kazi ya invetor ni kuubadili umeme toka kwenye dc(mkondo mnyoofi) kwenda kwenye ac(mkondo geu),endapo utawasha vifaa vyote ulivyo violozesha umeme utadumu kwa muda ule tulio ukadili mfano masaa 6 au s7,iweleke kwamba solar inategemea sana mahesabu na matumizi ya muitaji hivyo anafungiwa mteja kulingana na masaa na vifaa atakavyo viita vitategemeana
 
Back
Top Bottom