Mm Siyo mtaalam lakini kama ungeenda Kwa Msanifu Majengo bado angekuuliza Maswali.
1.Vyumba 3 Vyote Self,unataka vyoo vya Aina gani?Unataka na Kabati la nguo Ukutani?(Closet),Chumba Master Kwa wastani ni kuanzia Meta za Mraba 12 Hadi 20@
2.Unahitaji Sitting Room ya Ukubwa gani?Jiko na Dinning hall la Ukubwa gani? Canopy/Verandah?Car port ya ndani au nje?Store? Laundry?
Haya yote yatampa Taarifa aje na michoro pendekezwa kisha mshauriane.Hiyo ni floor plan.Toka hapo atakwenda kutengeneza mwonekano wa Nyumba ukiwa angani,au pembeni.Akimaliza kama utaridhia ataandaa michoro.Hii ukimpatia Quantity Surveyor atakupa hesabu ya Vifaa hitajika.Kisha Engineer wa Ujenzi au Fundi ataingia mpatane bei.
Kutegemeana na Mahali ulipo Gharama za Kujenga meta ya Mraba zinacheza Kati ya 150K Hadi 500K Kwa SQM.Kwa haraka haraka Vyumba 3 self,Sebule,Jiko,dinning,canopy,corridors na kadharika ni SQM Kati ya 100 Hadi 180.
Sasa zidisha hizo Kwa gharama ya Kujenga.Upande wa 2 ukipata gharama za Vifaa zidisha mara 35% Hadi 40% kupata gharama za Ufundi.Mfano kama Vifaa ni 50m zidisha mara 40% utapata 20m ya Fundi.Kila hatua ya ujenzi fundi au Mkandarasi atalipwa,mbali na Vifaa vya ujenzi.