Gharama ya vigae vya mbezi tiles

Gharama ya vigae vya mbezi tiles

Pafyum

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
208
Reaction score
113
Wana jamvi naomba kujua gharama ya vigae vya Mbezi tiles kwa mtu anaefaham, na pia uimara wake ukilinganisha na mabati ya gauge 28 ya migongo mipana! Pia kama ukiringanisha gharama za kuezeka kwa Vigae vya mbezi tilea na Mabati ya ALAF ya migongo mipana yapi ni expensive?

Natanguliza shukran zangu za dhati,
 
TEMBELEA KIWANDANI AU MADUKA YA JIRANI HUMU ALAF HAWAMO UNAPOTEZA MUDA WAKO KM KWELI unataka kujenga au kufungua duka
 
Naona uko mbali sana lakini ngoja nikujuze.

Ukitaka kuezeka kwa kigae inabidi katika ujenzi wako ulaze tofali badala ya kusimamisha kama tulivyozoea.

Kigae kinakula mbao nyingi sana na hata bei yake ni ghari hivyo kwa uchache ukitaka kuezeka kwa kigae bajeti yako isipungue 15ml kulingana na ukubwa wa ngumba.

Kwa mabati mengi kama ya South migongo mipana unaweza kuezeka kwa 8-9ml na huitaji kulaza tofali ili kukabili uzito wa bati kama ilivyo tofauti na kigae.

Huo ni kwa uelewa wangu mdogo wa ujenzi.
 
Mdau achana na vigae vya mbezi tiles. Tumia mabati ya south ambayo yanaonekana kama vigae. Yanapendezesha nyumba ile mbaya na bei yake ni poa kidogo kulinganisha na hivyo vigae. Nitumie email yako nikupe data zaidi kwani nimepitia huko tayari.
 
Nashukuru sna kwa usahuri wako, ndomana nikauliza wadau, maana unaweza ukawa unaogopa kuuliza bei ya samaki kwa kuangalia ukubwa wake kumbe anauzwa rahis! Unaweza ukanipa data hapa hapa jamvini kaka maana naamini si mimi tu ntakaefaidika na hizo data bali ni wengi ambao wanaogopa kuuliza bei ya samaki kwa kuangalia ukubwa wake
 
Naona uko mbali sana lakini ngoja nikujuze.

Ukitaka kuezeka kwa kigae inabidi katika ujenzi wako ulaze tofali badala ya kusimamisha kama tulivyozoea.

Kigae kinakula mbao nyingi sana na hata bei yake ni ghari hivyo kwa uchache ukitaka kuezeka kwa kigae bajeti yako isipungue 15ml kulingana na ukubwa wa ngumba.

Kwa mabati mengi kama ya South migongo mipana unaweza kuezeka kwa 8-9ml na huitaji kulaza tofali ili kukabili uzito wa bati kama ilivyo tofauti na kigae.

Huo ni kwa uelewa wangu mdogo wa ujenzi.

Umesomeka vizuri sana, endelea kutoa elimu kama hiyo kwani wengi darasa la ujenzi hatujalipitia.
 
Back
Top Bottom