Naona uko mbali sana lakini ngoja nikujuze.
Ukitaka kuezeka kwa kigae inabidi katika ujenzi wako ulaze tofali badala ya kusimamisha kama tulivyozoea.
Kigae kinakula mbao nyingi sana na hata bei yake ni ghari hivyo kwa uchache ukitaka kuezeka kwa kigae bajeti yako isipungue 15ml kulingana na ukubwa wa ngumba.
Kwa mabati mengi kama ya South migongo mipana unaweza kuezeka kwa 8-9ml na huitaji kulaza tofali ili kukabili uzito wa bati kama ilivyo tofauti na kigae.
Huo ni kwa uelewa wangu mdogo wa ujenzi.