Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Ili kukabiliana na gharama kubwa ya huduma ya dialisisi kwa wagonjwa wa figo, Serikali imeingiza nchini mashine mpya aina ya SWS 6000 ambazo zimewezesha zishuke kutoka Sh250,000 mpaka Sh150,000.
Mashine hizo moja ina thamani ya Sh31.76 milioni ambazo tayari zimefungwa katika hospitali za rufaa za mikoa. Zina uwezo wa kutoa huduma zaidi ya moja mgonjwa anapokua kwenye mashine na kutobagua vitendanishi.
Akizungumzia utendaji kazi wa mashine hizo leo Ijumaa, Desemba 27, 2024, muuguzi kiongozi wa kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, Abubakari Ali amesema mashine hizo zimeboresha huduma.
Amesema awali mgonjwa angeweza kupata changamoto kwenye mashine na ili kuitatua wangelazimika kusitisha huduma kwanza, lakini sasa utoaji huduma umeimarika.