Gharama za finishing

Gharama za finishing

TGD

Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
76
Reaction score
140
Mwenye uzoefu na gharama zifuatazo anambie nyumba ina vyumba vinne, jiko seble, vyoo viwili na bafu

Gharama ya plaster=
Kupaka rangi=
Wiring=
Plumbing=
Tiles=
 
Ndugu garama za ujenzi bila kuwa na ramani na vipimo hizo garama zitakuwa sio asilia

Tafuta ramani tuwasiliane nikutengenezee Boq itakayokupa muongozo idadi ya material unayohitaji na garama zake kwa ujumla
Nitafute 0657662776
 
Wewe ni fundi wa nn kati ya hizo mkuu
 
Mwenye uzoefu na gharama zifuatazo anambie nyumba ina vyumba vinne, jiko seble, vyoo viwili na bafu

Gharama ya plaster=
Kupaka rangi=
Wiring=
Plumbing=
Tiles=
Plasta ndani tu fanya kama laki 5 hivi au 6,
Ndani na nje fanya kama 1.2mil hivi Kwa nyumba kama yako.

Rangi ndani tu labda laki 5,
Ndani na Nje yaweza kua nayo 1.2m. Hii ni Ufundi tu. Materials itategemea. Rangi ya kuchanganya ndoo moja ni 180,000 kariakoo Plascon. Ndani ni silk na nje ni all weather. Bila kuchanganya ni kama 140,000/- hivi. Itategemea na Idadi ya ndoo pia ila ndani na nje hazipungui 6 jumla.

Wiring kutindua njia za kupitishia conduit pipes fanya kama 300,000. Hii ni pamoja na kuchimbia hizo pipes na boxes zake. Vifaa ni conduit pipes na boxes. Na akichimba Kwa mashine basi ongeza discs hapo.

Phase two ya wiring itakua kupitishia waya na hapo Ufundi kama laki 2 au 3 hivi. Vifaa ni main switch, Waya, switches, sockets, etc itategemea na mahitaji.

Plumbing napo kuchimba njia za mabomba na kuweka + kuunga hizo bomba ufundi ni kama laki 3 au 4 hivi. Vifaa itatagemea na Nyumba yako ilivyo ila kawaida sana andaa kuanzia laki 4. Hapa ni mabomba tu na connectors. Na akichimba Kwa mashine basi ongeza discs.

Baada ya hapo Kuna kuunga maji napo. Hii hutegemea source iko wapi.

Tiles hapo inategemea. Roughly box 1 la 40x40 zinakaa 12 lina cover 1.92sqm linauzwa 22,000 mpaka 25,000 Kwa dar bila usafiri. Piga hesabu nyumba yako ndani Ina eneo gani ni Sqm Kisha gawa Kwa 1.92 utakachopata kifanye kua number nzima Kwa kukadiria kwenda juu/mbele.

Hapo utapata idadi ya maboxi hitajika. Pia hizo SQM ukizidisha na alfu 5 utapat bei ya Ufundi. Assumption ni utatumia tiles za 40x40 kote.

Hapo utahitajika pia cement na mchanga kidogo.
 
Mwenye uzoefu na gharama zifuatazo anambie nyumba ina vyumba vinne, jiko seble, vyoo viwili na bafu

Gharama ya plaster=
Kupaka rangi=
Wiring=
Plumbing=
Tiles=
Ghalama za vifaa tu
Plaster andaa mifuko 70 + mchanga roli 5
Skimming powder mifuko 45
Rangi ndoo 3
Wiring andaa 2.5 m
Plumbing 2.3 m
Tiles andaa 4 m
Bei inaweza kupunguza au kuongezea kulingana na quality ya vitu utakavyotumia . Good luck
 
Mwenye uzoefu na gharama zifuatazo anambie nyumba ina vyumba vinne, jiko seble, vyoo viwili na bafu

Gharama ya plaster=
Kupaka rangi=
Wiring=
Plumbing=
Tiles=
Idadi ya chumba?
 
Mwenye uzoefu na gharama zifuatazo anambie nyumba ina vyumba vinne, jiko seble, vyoo viwili na bafu

Gharama ya plaster=
Kupaka rangi=
Wiring=
Plumbing=
Tiles=
Plumbing nione Mimi,kwa kazi nzuri na bei na vifaa Bora kabisa kwa bei nafuu
 
Nina nyumba ya vyumba vinne masta 2 na vya kawaida viwili. Niko kwenye finishing na mfuko hauruhusu kupambana nayo kwa wakati mmoja. Nimeona nianze na chumba kimoja kimoja kufanya finishing, mna ushauri gani ndugu zangu? Naomba kujuzwa garama ya finishing kwa master yenye ukubwa wa 4m by 4m. Wiring na plumbing tayari, plasta tayari, dirisha za grill tayari. Darini pia nishamaliza kupiga draft. Je naweza kupiga na tiles au nisubiri nimalize kwanza finishing ya vyumba vyote ndio niweke tiles? Shukran
 
Back
Top Bottom