Mwenye uzoefu na gharama zifuatazo anambie nyumba ina vyumba vinne, jiko seble, vyoo viwili na bafu
Gharama ya plaster=
Kupaka rangi=
Wiring=
Plumbing=
Tiles=
Plasta ndani tu fanya kama laki 5 hivi au 6,
Ndani na nje fanya kama 1.2mil hivi Kwa nyumba kama yako.
Rangi ndani tu labda laki 5,
Ndani na Nje yaweza kua nayo 1.2m. Hii ni Ufundi tu. Materials itategemea. Rangi ya kuchanganya ndoo moja ni 180,000 kariakoo Plascon. Ndani ni silk na nje ni all weather. Bila kuchanganya ni kama 140,000/- hivi. Itategemea na Idadi ya ndoo pia ila ndani na nje hazipungui 6 jumla.
Wiring kutindua njia za kupitishia conduit pipes fanya kama 300,000. Hii ni pamoja na kuchimbia hizo pipes na boxes zake. Vifaa ni conduit pipes na boxes. Na akichimba Kwa mashine basi ongeza discs hapo.
Phase two ya wiring itakua kupitishia waya na hapo Ufundi kama laki 2 au 3 hivi. Vifaa ni main switch, Waya, switches, sockets, etc itategemea na mahitaji.
Plumbing napo kuchimba njia za mabomba na kuweka + kuunga hizo bomba ufundi ni kama laki 3 au 4 hivi. Vifaa itatagemea na Nyumba yako ilivyo ila kawaida sana andaa kuanzia laki 4. Hapa ni mabomba tu na connectors. Na akichimba Kwa mashine basi ongeza discs.
Baada ya hapo Kuna kuunga maji napo. Hii hutegemea source iko wapi.
Tiles hapo inategemea. Roughly box 1 la 40x40 zinakaa 12 lina cover 1.92sqm linauzwa 22,000 mpaka 25,000 Kwa dar bila usafiri. Piga hesabu nyumba yako ndani Ina eneo gani ni Sqm Kisha gawa Kwa 1.92 utakachopata kifanye kua number nzima Kwa kukadiria kwenda juu/mbele.
Hapo utapata idadi ya maboxi hitajika. Pia hizo SQM ukizidisha na alfu 5 utapat bei ya Ufundi. Assumption ni utatumia tiles za 40x40 kote.
Hapo utahitajika pia cement na mchanga kidogo.