Gharama za Kuanzisha Website ya Biashara 2020 (Mwongozo Rahisi)

Charge hiyo kila mwaka unalipa kuendesha biashara mtandaoni,
Binafsi sijawahi isikia hiyo, ndugu. Ninachofahamu ukishasajili your business once it's over. You just play with taxes.
 
Hiyo template ndo wordpress au?
Hapana, template ni website ambayo imeshatengenezwa tayari kwa ajili ya matumizi ya wengi (ambayo inaweza kutengenezwa kwa mfumo wowote) wewe unaichukua hiyo na kuanza kuifanyia marekebisho kulingana na mahitaji yako.

Yani kama unavyonunua Totoya IST mpya then unaifanyia mabadiliko kulingana nawewe upendavyo ionekana. Lakini IST haikutengenezwa maalum kwa ajili yako ila kwa ajili ya wengi.
 
Anhaa na wordpress inafanyaje kaz?
Wordpress ni CMS (Content Management System), ina maana inakusaidia ku manage content uliyo nayo ambayo unahitaji kuiweka kwenye mfumo wa kidigitali au mtandaoni.

Lakini haishii hapo tu Wordpress inauwezo wa Kukusaidia kutengeneza Websites kwa kutumia njia mbali mbali: Codes, Template, Website Builder (Plugins) .... In short wordpress ni Software kubwa inayosaidia ku manage Content yako unayotaka kuiweka mtandaoni kwa namna yoyte na inafanya zaidi ya hayo. Ni tool kubwa mno.
 
Ukishaitengeneza sasa unaipelekaje online?Hapo tuseme tayari una domain
Unatakiwa kwa uwe na Hosting, then kwenye hosting wanakupa kitu kinaitwa Cpanel, huko ndiko una upload your code files na zitaonekana mtandaoni.
 
anhaa...na watu wa blog wanapitia hizi process kweli?
Wapo wanaotumia njia hizi ambao wako advanced kidogo ... Ila kwa technology ya sasa huitaji kujua coding ili kutengenza blog au website kuna tools zaidi 20 zinazowez kukusaidi kufanya hiyo kazi kwa kutumia mtindo wa drag and drop. Mfano, Wordpress, Webflow, Wix, Editor X, Squrespace na nyingine nyingi.
 
sawa mkuu...ishu ya domain and hosting kwa upande wa blog inakuwaje?
Unanunua tu mtandaoni kama kawaida, kupitia kampuni zinazotoa Hizo service kama Namecheap, na wengineo wengi. Just Google tu ni ishu rahisi zaidi.
 
i like you uko vizuri web design wewe umespedify kwenye nini hasa au ndio web and graphics design
 
kaka mimi nina maswali mawili je naweza kutumia inspect elemnt ku copy na ku create website yangu na je naitaji kujua computer language ngapi ku create webside mbali na HTML .
 
kaka mimi nina maswali mawili je naweza kutumia inspect elemnt ku copy na ku create website yangu na je naitaji kujua computer language ngapi ku create webside mbali na HTML .

Hapana, hicho kitu ni ngumu kwa miaka ya sasa kwa sababu, most of the codes, kwenye inspect tool zinakuwa zimezuiwa kuonekana, hivyo utakuwa unapoteza muda ukifanya hivyo, ... ila unaweza kutumia inspect tool kuona feature flani ambayo ipo kwenye website ukaelewa kidogo namna ya wewe kuifanya pia.

Solution, ni ku-search Google HTML templates, hizo zinakuwa zina faili kamili, utazidownload na kuzitumia kujenga web yako.

Swali la pili: Mbili tu HTML na CSS inatosha, but kama unataka iwe nzuri zaidi jifunze na JAVASCRIPT.

- Pia unaweza kujifunza lugha kama Flutter ambayo yenyewe ukijua tu peke yake unaweza kujenga kitu kizuri.

Note that: Sio lazima ujue Coding ili kutengeneza website kwa miaka ya leo. Infact, coding itakufanya uchukue muda zaidi kujenga website simple tu ambazo ungejenga hata kwa Wix au Wordpress.
 
yeah thanx brother ingawa java ni ndefu but i will try for fun.
 
Vizuri sana mkuu nidizainie application kwa ajili biashara yangu ya matunda. Yani inakuwa kama uber vile. Mteja akitaka Matunda basi application ndo ifanye kazi ya kutukutanisha. Sina ela nyingi sana nina misimbazi mitatu tu. By the way hongera sana tafuta scholarship uende nje ukajifunze zaidi.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Pia kama waweza nishauri kuhusu biashara yangu ya chakula je naweza kuiundia web? Kuhusu matunda ukinisaidia kuandaa hiyo application na kuwa verifaid play store utakuwa umesapoti sehemu kubwa sana ya hastlle zangu bro.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 

Mmh kaka mimi nisikudanganye, hicho kiasi kwa application hakitoshi hata kidogo, kwa sababu kima cha chini kabisa ili kutengeneza application nzuri kwa ufahamu wangu sio chini ya 1M, kama kweli unahitaji kitu cha kudumu na kuna wababaishaji wengi wataongea kuwa inawezekana kutengeneza app kwa 300k au hata 50k ... Lakini kwa experience yangu utakuwa unapoteza fedha na hutoweza kutatua tatizo unalohitaji hiyo application itatue.

Ushauri wangu hiyo fedha ni kheri, uiongeze kidogo tu. Utengeneze Website kwa kutumia template na hosting ya bei rahisi. Website itaweza kukusaidia kukusanya hizo oda pia kama unavyohitaji tena inaweza kuwa bora kuliko app. Kwa sababu hakuna habari ya kutumia data kudownload. Na tena ukitengeneza brand yako vizuri kupitia social media watu watakuwa wanaoda bila kuanza kwenda kudownload app ila wataingia kwenye website chap na kumaliza shughuli zao.

Mi nitakusaidia kukupa ushauri tu bure, ila kwenye suala la kuifanya hiyo kazi bajeti yako mkuu, sidhani kama itafaa muda wangu nisamehe kwa hilo. Nashkuru pia kwa kunitakia mema kuhusu scholarship, ila kwa upande wangu naamini katika kujiendeleza mwenyewe kupitia experience ya kufanya kazi halisi.
 
Inawezekana kubadili template website kuwa custom website?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…