Inategemeana na mfuko wa hela yako ulivyo na sehemu unayotaka kufungua hiyo barbershop yako, uwe na fedha za kukodi flemu, kwa kukisia flemu haizidi 200,000/=, vifaa mara nyingi huanzia shs 150,000/= na vifaa vingine vinazidi 1,500,000/= sasa inategemea kapu la mfuko wako ulivyo,
Iinaitajika uwe na kinyozi mwenye ujuzi wa kutosha na stadi wa kazi, na uwe na mdada wa kufanya massage kwa wateja wataoingia katika hiyo barbershop yako, kwani itavuta wateja wengi kuja hapo na kupata income unayotaka. kama utakuwa na uwezo wa vitu vyote hapo basi unaweza anzisha hiyo barbershop yako