Gharama za kutoa gari bandari

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,527
Reaction score
3,811
Habari wakuu,

Kuna kibaby walker niliagiza, sasa kimefika. Nimeongea na kampuni ya clearing wamenipa hizi gharama ukiachana na kodi ya TRA ambayo naweza kuona kwenye system ya TRA, ningependa kujua uzoefu wenu kama zipo sawa mana nadhani mnajua hapa mjini ujanja ujanja mwingi. Gharama hizo ni; Shipping lines 150,000 Wharfage 115,000 Port charges 250,000 Plate number 50,000 na Agency fee ni 300,000

Naombeni uzoefu wenu wakuu
 
Sawa lipia ukachukue Kibaby Walker

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
Kibaby walker ndio Gari ya Aina Gani?
 
Bro ukifanikiwa utuambie hako ka baby walker kamekugharimu kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu bei hazijakaa sawa hasa kwenye upande wa plate number na agency fee. Bei ya plate number ni tsh. 30,000 na agency fee bei ya soko ya ku-clear saloon car ni tsh 200,000 mpaka tsh. 250,000.

Karibu katika kampuni yetu, agency fee tutakutoza tsh. 200,000 tu, tunafanya kazi kwa uaminifu, ufanisi na kwa haraka.

Tunapatikana kwa anuani ifuatayo;

S.A Link Traders Ltd (Clearing & Forwarding Company)
2nd Floor-Elite City building (Opposite Harbor View),
Samora Avenue/Morogoro Road,
Dar es Salaam- Tanzania.
Email: info@salink.co.tz
Mob: +255718 866 651 ( Call or Whatsapp )
Website: www.salink.co.tz
Facebook page: S.A LINK Traders LTD
 
Kumbe plate namba nayo unalipia mimi nikajua ndio ile regstration fee oliyopo katika kodi ya TRA ukiview kwenye Calculator

Sent using Jamii Forums mobile app
Registration fee ni kwa ajili ya kupata kadi ya gari tu, plate number inanunuliwa kwenye makampuni ya sign industries kama Kiboko, Masasi n.k.
 
Duuh agency fee ndo kakunyoosha ila inakuwanga ni makubaliano sio fixed kama mlikubaliana hivyoo sawa huko kwingine akiokota twenty twenty sio mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…