Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 18,772
- 8,939
Habari zenu wadau
Ninaitaji kufahamu jumla ya gharama za kutoa gari bandarini, aina ya Nissan X trail ya mwaka 2007.
Ina 1990cc.
CIF price Ni USD 6361.
| Make: | NISSAN | |
| Model: | X-TRAIL | |
| Body Type: | SUV | |
| Year of Manufacture: | 2007 | |
| Fuel Type: | PETROL | |
| Engine Capacity: | 1001 - 2000 CC | |
| Customs Value CIF (USD): | 5164.00 | |
| Import Duty (USD): | 1291.00 | |
| Excise Duty (USD): | 322.75 | |
| Excise Duty due to Age (USD): | 968.25 | |
| VAT (USD): | 1394.28 | |
| Total Taxes (USD): | 3976 | |
| Total Taxes (TSHS): | 7128968 |
Una hakika?
Last May niliagiza gari nikakutana nayo...
Ndio nina uwakika, naagiza mara gari mara nyingi,
Siku hizi hakuna mambo ya kukadiria, kila kitu kipo wazi kwenye FOMULA.
haata gari lako ukipewa bure au zawadi au ukinunua mabilioni fomula ni moja Ndugu yangu.
Nenda page ya TRA kuna excel sheet ina kila kitu. Wana bei ya kila gari likiwa mpya. Unaingiza mwaka wa gari, bei ya gari husika na diprisiesheni factor kwa asilimia. Then unapata cost zote in USD. Ukiingiza exchange rate ya siku husika utapata on Tshs. Hiyo CIF yako haina lolote kwenye calculations zao
Utaratibu umebadilika lini....
Sikun nyingi utaratibu ndio huo, tokea waanze kutumia FOMULA hakunaga tena longolongo.
na ndivyo ilivyo kwa wajanja tunajitahidi unapoagiza gari CIF iwe kubwa kuliko KODI maana ni bora kununua gari zuri kwa bei mbaya kuliko gari baya kwa bei rahisi na kuja kuwachangia KODI MAFISADI.
Unatia mashaka mkuu....
Hiyo calculator naijua....ila inatumika tu endapo bei yao ni kubwa kuliko bei yako!
Mkuu naona kama unabisha tu.
RR agent wako alikulisha tango pori. Alitakiwa arekebishe invoice isome kama cif ya kwenye database inavyosema. Njoo kwa maprofessional kwenye industry hii tukufanyie kazi yako fair.
Abra One cif means Cost, Insrance na Freight. Kiswahili maana yake ni gharama ya mzigo, bima ya mzigo ukiwa melini au kwenye ndege au usafiri wowote utakao tumia na gharama ya usafirishaji (nauli)
CIF ni nin wapendwa?
Kibanga hizo bei unazoweka hapo hazina registration na other charges. Utawalisha watu tango pori
Wewe kibanga unapotosha watu. Unapoongelea swala linalohusu hela especially ushuru inabidi ukamilishe mahesabu. Mpe mtu gharama zote kama tansad itakavyotoka. What if huyo mtu aweka budget ya 3.4m halaf inakuja kuongezeka kwenye tansad?? Nakufundisha tena unapompa mtu estimation ya kodi hakikisha umeweka na gharama ya registration na psi ya tra.
Hasante sana Mkuu, naomba mwongozo wako juu ya gari tajwa hapo juu, uwezo wa kuhimili mikiki mikiki, ulaji wa Mafuta, mwingiliano wa spare na magari mengine, upatikanaji wa spare na bei zake.