Gharama za maegesho kuanza kulipwa kwa njia ya mtandao

Gharama za maegesho kuanza kulipwa kwa njia ya mtandao

ngoshamaguzu

Member
Joined
Jul 12, 2020
Posts
25
Reaction score
44
Natumaini mko vizuri mnapambana kutafuta riziki

Ngoja nijikite moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Leo trh 23 aug 21 kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa dar imetoa maelekezo ya kuanza kutumika kwa mfumo wa ulipaji gharama za kupaki magari kwa njia ya kielectroniki ambapo mitandao yote ya simu itatumika katika malipo hayo. Ambapo itaanza rasmi tarehe 1 sept 2021

Binafsi Imenishitua kutokana na uwepo wa ongezeko la tozo za ulipaji au utumaji pesa. Ila ombi langu kwa watendaji kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kutoa maelekezo ya kuanza kwa utekelezaji.

Naomba kuwasilisha.

Maegesho.JPG
 
Jambo zuri sana ingawa tumechelewa…..wenzetu nairobi walianza siku nyingi sana.
 
Natumaini mko vizuri mnapambana kutafuta riziki

Ngoja nijikite moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Leo trh 23 aug 21 kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa dar imetoa maelekezo ya kuanza kutumika kwa mfumo wa ulipaji gharama za kupaki magari kwa njia ya kielectroniki ambapo mitandao yote ya simu itatumika katika malipo hayo. Ambapo itaanza rasmi tarehe 1 sept 2021
Kwa hiyo wageni wa muda wasio na namba ya Tanzania hawatalipa?

Kuna wakati nilienda Nairobi nikakodi gari ya pale nikakuta wameifunga. Nikawaambia mie mgeni sina namba ya Kenya kwa hiyo ningelipaje?
 
Mimi naunga mkono ila waweke tozo zinazoendana na kipato cha watu walio wengi na sio zinazoendana na wachache. Na ziwe sawa kwa majiji yote kwani kila jiji likisha achiwa kujiwekea utaratibu/tozo ndio hapo mambo huanza kuharibika.
Hai ingii akilini kuwa mkazi wa Dodoma anauweo wa kulipa kuliko Dar au pengine mkazi wa Arusha anauwezo wa kulipa kuliko Dar wakati wote wapo miini na wote wanajishuhukisha pengine waajira wa kazi zinazofanana
Wanaweza kuweka penigine makundi matatu
1hr shs 300
2hrs shs 600
3hts to 12hrs - 1000
 
Back
Top Bottom