Gharama za meno bandia na bima ya afya- NHIF

mwambojoke

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
1,084
Reaction score
647
Naomba kuuliza wana jukwaa hili.

Je, Bima ya Afya ina cover ukihitaji kubadili meno na kuweka ya bandia? Ama ni hospitali zipi na kwa gharama zipi naweza pata huduma hii kwa Dar es salaam?
 
Hakuna hilo fao la anasa
Labda matibabu tu ya kinywa na meno
 
Meno bandia NHIF inalichukulia kama anasa kwa hiyo jipange kwa hela yako. Muhimbili kipo kitengo cha meno!
 
Nenda pale muhmbili mwenywe ukajionee uchague na meno yanayoendana na wew.
 
Kuyasugua je? Yangu yanakuwa na rangi
 
Mimi nauliza kuhusu hospital gan naweza kupata huduma ya jicho la bandia na gharama ni kiasi gani maana nilpata ajali
 
Chukulia hata mkopo ndugu,meno sio anasa ni kitu muhimu kama vidole katika mwili n.k.Ukiwa na pengo huwezi kutafuna vizuri,huwezi kuongea vizuri,ukiongea mate yanatoka bila mpangilio,ulimi nao unakuwa hauchezi mbali na hiyo sehemu yenye pengo hivyo kumfanya mtu aonekane kila wakati kama anatafuna jojo,yaani ni sheeeda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…