Ndugu wana jukwaa,
hii miito ya simu (wengine wanaita hello tunes etc) mbona kujitoa ni vigumu kiasi hiki, sasa hivi wananiambia kuna muziki wanataka "kuRENEW" sasa najaribu kujitoa inashindikana, je ni halali kwa hawa jamaa kukata pesa za mlaji "automatically" bila mteja kukubali au kukataa? mbona kwenye M-pesa kuna meseji inasema bonyeza moja kukubali au mbili kukataa?
au ukivutiwa na nyimbo unayoisikia kwa jamaa uliyempigia ukalogwa na kubonyeza nyota(*) umeingia mkataba wa milele kukatwa pesa?
Sheria ya nchi yetu inasemaje?
Namba msaada wenu wadau, hii kero inanitesa sana na lakufanya sijui