Gharama za rh disease

Lundavi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Posts
327
Reaction score
324
Samahani wadau, mke wangu kaharibikiwa na mimba mbili, baada ya kufanya vipimo ikagundulika kuwa makundi yetu ya damu hayafanani kwasababu mke wangu ana o- na Mimi nina o+ hivyo hupelekea mimba kutoweza kustahimili due to blood type incompatibility. Dactari aliyetufanyia vipimo anasema tatizo hilo hutibiwa kwa mke kuchomwa sindano inayofifisha reaction ya kinga ya mama kwa kiumbe kilichopo tumboni. Kwa maelezo ya daktari ni kwamba wanawake wenye kundi la damu o- huwa na uwezo mkubwa wa kujikinga na magonjwa, hivyo mimba inapotungwa mwili huichukulia kama ugonjwa hivyo hupambana nayo na kupelekea kuharibika. Daktari anadai tiba hiyo(ya sindano) ni ghali sana hivyo naomba mwenye ufahamu wa gharama za tiba hiyo anifahamishe kwa msaada. Natanguliza shukrani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…