Gharama za uendeshaji benki kuwaumiza wafanyabiashara

Gharama za uendeshaji benki kuwaumiza wafanyabiashara

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
Ongezeko la gharama za uendeshaji wa benki na masharti mapya ya kodi yaliyowekwa na serikali kwa taasisi za fedha yameathiri yametajwa kuathiri mwenendo wa utoaji mikopo kwa wafanyabiashara nchini.

Ongezeko la gharama za kuendesha benki linachangiwa na kupungua mzungo wa fedha ambao ni matokeo ya kupungua kwa amana za serikali zilikuwa zinawekwa katika benki hizo. Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani iliamuru taasisi zake kuhamishia akaunti zao Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa madai ya kuthibiti matumizi ya fedha za umma.

Mabadiliko hayo katika sekta ya fedha yaliathiri mwenendo wa ukopeshaji katika benki mbalimbali ambapo benki zimeongeza riba ili kufidia gharama za kuendesha shughuli zao.

Ripoti ya mapitio ya uchumi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwezi Oktoba mwaka huu, inaeleza kuwa katika nusu ya pili ya mwaka 2017 riba inayotozwa kwenye mikopo ya benki imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2016.

Ripoti hiyo inafafanua kuwa riba iliyotozwa kwenye mikopo kwa mwezi Septemba 2017 imeongezeka hadi kufikia asilimia 18.46 kutoka asilimia 17.46 mwezi Agosti ikilinganishwa 15.83% ya mwezi kama huo mwaka 2016.

Ongezeko la riba limetajwa kupunguza idadi ya wateja wanaokopa na kuathiri sekta za kilimo, ujenzi, mawasiliano na usafiri ambazo zinategemea mikopo kutoka benki kuendesha shughuli zao. Ili kukabiliana na hali hiyo benki zimepunguza riba kwenye amana zinazowekwa katika benki zao ili kuvutia wateja wengi zaidi kuwekeza fedha katika taasisi hizo.

Ripoti hiyo ya BOT inaonyesha kuwa mwezi Septemba 2017, riba iliyokuwa inatozwa kwa amana za benki ilipungua zaidi kuliko mwezi uliotanguliwa wa Agosti, na riba hiyo ni kubwa ikilinganishwa na mwezi kama huo 2016. Kutokana na hali ya kiuchumi uwezekano wa riba hiyo kupungua ni mkubwa kwa siku zijazo.

Zaidi, soma => Gharama za uendeshaji benki zinavyoathiri utolewaji wa mikopo kwa wafanyabiashara | FikraPevu
 
Back
Top Bottom