Gharama za Ushuru wa gari Bandarini

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2008
Posts
2,268
Reaction score
335
Salama wakuu,naombeni msaada kwani kuna rafiki yangu yuko kwa Bibi (Uingereza) anataka kunitumia gari la kutumia hapa mjini.ni Toyota Collora 1997, Milango mitano(Saloon), lakini gharama za kuikomboa gari Bandarini ni juu yangu,Kwa hiyo naomba kujua Gharama za kuikomboa hapa Bandarini (Dar) natanguliza shukrani.
 
Msaada please!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Bora uende tra utapata jibu kamili! Ila nina wasiwasi garama itakua juu sababu ni ya miaka zaidi ya kumi
 
Bora uende tra utapata jibu kamili! Ila nina wasiwasi garama itakua juu sababu ni ya miaka zaidi ya kumi
Mkuu niko huku mkoani nimetingwa na shughuli.Ndo nikaamua kutumia huu mtandao ili kurahisisha kazi.
 
Huu mpango ufanye na mawakala wa kutoa mizigo bandalini, labda ungeni pm ningekupa namba zao, hawa watu wanajua how to deal na situation hizi, natumai una bahati kwa kuliingiza gari lako kutokea uingereza, kwani nasikia makadilio ya kodi kwa magari toka uingereza inakuwa ngumu kwa tra kwani wanakosa exactly value yake ktk mtandao ivo wanakukadilia tu.... Kuna kitu kama hicho.
Duh lakini pia gari ya 1997 nadaut km utaepuka kodi inayoitwa uchakavu, tra wakiona 1997 wanaanza kusherehekea kabisa, lakini uliza zaidi
lakini pia mwanagu ungelitoa japan ungekoma, hata kama umebargain bei uko Japan wakakupa discount likifika bongo wanalipandisha bei ipasavyo na unabamizwa 52% km kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…