Gharama zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), endapo mtu akitaka kubadili umiliki wa gari zipoje?

Gharama zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), endapo mtu akitaka kubadili umiliki wa gari zipoje?

kakamgeni

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2018
Posts
241
Reaction score
201
Wakuu Bila Shaka Mtakuwa Mnaendelea Vyema Na Mchakato Wa Kusukuma Gurudumu La Maisha. Kwa Upande Wangu Namshukuru Mwenyezi Mungu Naendelea Vizuri Kabisa.

Uzi Huu Nimeuleta Kuhitaji Ufafanuzi Kuhusu Gharama Zinazotozwa Na Mamlaka Ya Mapato Tanzania(T.R.A), Endapo Mtu Akitaka Kubadili Umiliki Wa Chombo Na Matumizi.

Labda Nitolee Mfano Mdogo Wa Gari Kama Vile Vitz Ambayo Umeinunua Kwa Milioni 4 Kamili, Ukawa Umekamilisha Vigezo Vyote Vinavyotakiwa Kwa Ajili Ya Kufanya Zoezi Zima La Kubadili Umiliki Na Matumizi, Masalani Gari Ilikuwa Ya Biashara(Uber), Hivyo Unataka Kutoa Kwenye Commercial Kwenda Private Kisha Ubadili Na Jina.

Kwa Anaefahamu Gharama Nzima Ya Zoezi Hilo Husika, Ningependa Anifahamishe, Kwa Mfano Mdogo Wa Gari Kama Hiyo. Naamini Kwenye Wengi Kuna Mengi, Asante Sana Nawasilisha.
 
Kisheria unatakiwa ulipe Gharama za kubadili kadi ambazo ni 10000(sina hakika Kama haijabadilika),utatakiwa pia ulipe 1% ya bei ya manunuzi ya gari husika kulingana na mkataba wenu.

Hapo kwenye 1% Ndio kuna changamoto,huwa hawakubali bei mlioandikiana ktk mkataba,hivyo hufanya tathmini upya na Gharama huongezeka kidogo
 
Asante Sana
 
Usijali nenda na laki mbili ambayo haitaisha na tena kama ukikomaa mwenyewe bila kutumia madalali inaweza isifike hata laki kikubwa uwe na mkataba halali ambao wa mwanasheria
 
Back
Top Bottom