Ghasia za Capitol: FBI yaonya wafuasi wa Trump huenda wakazua ghasia zaidi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa rais.

Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa kwake Januari 20.

Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Siku ya Jumatatu Bw. Biden aliwaambia wanahabari kwamba haogopi kula kiapo chao urais nje ya bunge la Marekani.

Yeye pamoja makamu wake mteule Kamala Harris bado wanatarajiwa kuapishwa nje ya jumba la Capital Hill, wiki mbili baada ya eneo hilo kuvamiwa na wafuasi sugu wa Rais Trump wanaopinga matokeo ya uchaguzi.

Maafisa wa usalama wamesisitiza hali iliyoshuhudiwa Januari 6 haitarudiwa tena- baada ya maelfu ya wafuasi wa Trump kufanikiwa kuingia katika majengo hayo wakati wabunge walikuwa wakipiga kura kuidhinisha matokeo ya uchaguzi.

Chad Wolf, kaimu mkuu wa wizara ya usalama wa ndani, siku ya Jumatatu alisema ameagiza shirika la Upelelezi la Marekani kuanzisha oparesheni maalum ya maandalizi ya kumuapisha rais mpya Jumatano - siku sita kabla ya hafla yenyewe - "kutokana na tukio la wiki iliyopita linaloegemea masuala ya usalama. "

Maafisa wanasema hadi wanajeshi 15,000 wa kitaifa huenda wakatoa ulinzi wakati wa hafla hiyo.

Baadaye siku hiyo ya Jumatatu, Bw. Wolf alikuwa waziri wa tatu wa Trump kujiuzulu tangu kutokea kwa maandamano dhidi ya bunge, baada ya Betsy DeVos na Elaine Chao.

Kuondoka kwa Bw. Wolf kuliiweka wizara yake katika hali ya ngumu wakati inapojiandaa kusimamia usalama wakati Biden atakapoapishwa. Wiki iliyopita Bw. Wolf alitoa wito kwa Bw. Trump "kuwalaani vikali" waandamanaji waliovamia bunge.

Wazir huyo anayeondoka alisema hatua yake imechangiwa na "matukio ya hivi karibuni", ikiwa ni pamoja na maamuzi ya korti kupinga uhalali wa uteuzi wake kisheria.

Ni maandamano gani mengine yanapangwa?

Maafisa wa usalama wanasemekana kujiandaa kote nchini kuhusu uwezekano wa ghasia zaidi kutokea siku chahche kabla ya Joe Biden kuingia rasmi madarakani.

Ujumbe kutoka kwa mtandao wa wafuasi wa Trump na wale wa mrengo wa kulia umetoa wito wa maandamano katika miji kadhaa Januari 17 na matembezi kuelekea Washington DC siku ya kuapishwa rais mpya na makamu wake.
 
ingekua Tiss ndio wamezuia wafuasi wa chadema

Wapumbavu wangesema Tiss inatumika na serikali
 
Trump is mad,he can't get the chance to rule USA any more.

"We can't breathe"
 
Hiyo ingetokea kwetu basi wangesema vyombo vya usalama vinafanya kazi kwa ajili ya chama.

Lakini mradi ni wazungu basi ni sawa tu.

Subiri uone majibu yao hao africans.
 
Waache waandamane ndiyo demokrasia wanayotuhubiria wakiwauwa itabidi mataifa ya ulaya wayawekee vikwazo
 
Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa rais.

Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa kwake Januari 20.

Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Siku ya Jumatatu Bw. Biden aliwaambia wanahabari kwamba haogopi kula kiapo chao urais nje ya bunge la Marekani.

Yeye pamoja makamu wake mteule Kamala Harris bado wanatarajiwa kuapishwa nje ya jumba la Capital Hill, wiki mbili baada ya eneo hilo kuvamiwa na wafuasi sugu wa Rais Trump wanaopinga matokeo ya uchaguzi.

Maafisa wa usalama wamesisitiza hali iliyoshuhudiwa Januari 6 haitarudiwa tena- baada ya maelfu ya wafuasi wa Trump kufanikiwa kuingia katika majengo hayo wakati wabunge walikuwa wakipiga kura kuidhinisha matokeo ya uchaguzi.

Chad Wolf, kaimu mkuu wa wizara ya usalama wa ndani, siku ya Jumatatu alisema ameagiza shirika la Upelelezi la Marekani kuanzisha oparesheni maalum ya maandalizi ya kumuapisha rais mpya Jumatano - siku sita kabla ya hafla yenyewe - "kutokana na tukio la wiki iliyopita linaloegemea masuala ya usalama. "

Maafisa wanasema hadi wanajeshi 15,000 wa kitaifa huenda wakatoa ulinzi wakati wa hafla hiyo.

Baadaye siku hiyo ya Jumatatu, Bw. Wolf alikuwa waziri wa tatu wa Trump kujiuzulu tangu kutokea kwa maandamano dhidi ya bunge, baada ya Betsy DeVos na Elaine Chao.

Kuondoka kwa Bw. Wolf kuliiweka wizara yake katika hali ya ngumu wakati inapojiandaa kusimamia usalama wakati Biden atakapoapishwa. Wiki iliyopita Bw. Wolf alitoa wito kwa Bw. Trump "kuwalaani vikali" waandamanaji waliovamia bunge.

Wazir huyo anayeondoka alisema hatua yake imechangiwa na "matukio ya hivi karibuni", ikiwa ni pamoja na maamuzi ya korti kupinga uhalali wa uteuzi wake kisheria.

Ni maandamano gani mengine yanapangwa?

Maafisa wa usalama wanasemekana kujiandaa kote nchini kuhusu uwezekano wa ghasia zaidi kutokea siku chahche kabla ya Joe Biden kuingia rasmi madarakani.

Ujumbe kutoka kwa mtandao wa wafuasi wa Trump na wale wa mrengo wa kulia umetoa wito wa maandamano katika miji kadhaa Januari 17 na matembezi kuelekea Washington DC siku ya kuapishwa rais mpya na makamu wake.
Lissu bingwa wa katiba,haki za binaadamu na sheria yuko wapi.

Mzee Amsterdam huoni madili huko mkuu
 
Dunia ya sasa ni vijana. Vijana unapo watisha-tisha ndio unawapandisha mori zaidi wa mapambano! Busara itumike. Hali itakuwa mbaya sana. It is obvious magaidi wa Kiarabu wataingia, na watakaribishwa kwa mikono miwili. Walikuwa wanaisubiri fulsa kama hiyo kwa hamu kubwa sana. Now it is bingooooo!!!!
 
Back
Top Bottom