Ghati Zephania Chomete ashiriki uzinduzi wa daraja la mto Mori & Wamaya

Ghati Zephania Chomete ashiriki uzinduzi wa daraja la mto Mori & Wamaya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum kutokea Mkoa wa Mara Ghati Zephania Chomete tarehe 01 Machi 2023 ameshiriki Mkutano wa Uzinduzi wa Daraja la Mto Mori & Wamaya Katika Kata ya Kirogo Wilayani Rorya Mkoani Mara. Madaraja hayo yamegharimu zaidi ya Shilingi za kitanzania Bilioni 1.5.
WhatsApp Image 2023-03-02 at 18.49.59.jpeg


Ikumbukwe kuwa katika Mkutano wa 10, Kikao cha 1 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ghati Zephania Chomete (Mb)-Viti Maalum Mkoa wa Mara aliwasilisha Taarifa ya Mwaka mmoja kuhusu Shughuli za Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Januari 31, 2023.

WhatsApp Image 2023-03-02 at 18.49.59(1).jpeg

Wananchi wa Mkoa wa Mara kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakisema kuwa Chomete ni kiongozi muadilifu, wametoa maoni yao na kumuombea mema Chomete kwani amekuwa akifanya vizuri katika kazi zake za kibunge.
 
Nyie chawa mna tabu sana.
Sasa hapo huyo kachapa kazi gani hadi kusifiwa?
 
Leta picha ya madaraja badala ya kuleta picha Ghati...shida kwelikweli au lengo la mtoa Mada ni kufikisha picha ya Ghati.
 
Mleta mada ni moja ya products za CCM zilivyo katika ubora wake.
Yaani ukimsoma tuu unajua chama hicho kilivyo na watu "very genius" chini ya Katibu mkuu wao Mheshimiwa Chongolo aliye agiza kuwa watu wakimakiliza masomo na kupata degree zao waende VETA kusoma ufundi ili kujiajiri.
Kuendelea kuwa na CCM baada ya 2025 ni sawa na taifa kukumbwa na Tufani
 
Back
Top Bottom