Mkurugenzi pole kwa uchovu wa kazi, najikita moja kwa moja kwenye hoja, mkurugenzi nimeamua kukuandikia barua hii ya wazi nikikupa taarifa kuhusu utiririshaji wa maji machafu ya chooni yanayotoka kwenye ghorofa za shirika la nyumba (NHC) zilizopo hapo Ubungo Shekilango Dar es salaam.
Septic tank zao zimezidiwa na kupasuka na kuachia mfereji wa maji machafu ya chooni yakielekwa barabarani kupitia kwenye kituo Cha mabasi ya mwendokasi kipya cha Shekilango ambacho hakijaanza kutumiwa na mabasi hayo, kwa sasa kinatumiwa na mabasi ya daladala .
Ni matumaini yangu kwamba utalishughulikia suala hilo ambalo ni zaidi ya mwaka sasa bado harufu zinasumbua wananchi, na sipati picha kama hilo tatizo lingesababishwa na nyumba ya mtu binafsi jinsi ambavyo mgemkomalia.