Gidabuday ashusha waraka mzito, amvaa Bayo

Gidabuday ashusha waraka mzito, amvaa Bayo

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Nathibitisha kwamba nimeanza taratibu za kisheria kutafuta haki ya Kikatiba kuhusiana na utata wa vigezo vya John Gilbert Bayo kuendelea kuhodhi nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Nimesimamia hilo kwakua nilisema mara kadhaa na hakuna alienipa sababu za msingi kwanini halishughulikiwi au kwanini niache kuendelea kulizungumzia. Labda angetokea kiongozi kuniambia Gida hili swala liache kwasababu 1, 2, 3 mimi ningeheshim na kuacha, lakin ukimya unaleta mashaka sana labla kuna jambo kubwa linaendelea tusilolijua na ndio maana nimeamua kulivalia njuga ili kama kuna lolote liwe wazi basi.

Ni muhimu kutofungia macho maswala ya kughushi vyeti, BMT walisema wanafuatilia uhalali wa vyeti lakini ninahakika hawanyi lolote bali wanavuta muda wakiamini kelele zangu na za wadau wa riadha zitaisha na jamaa yao amalizie muda wa miaka minne.

BMT na Mkurugenzi wangetaka kulifuatilia wangetumia masaa wala siyo masiku wala miezi; hili jambo linawahusu wao wote, namsikitikia Mhe Waziri Bashungwa (siyo Gekul) maana bado wanamuaminisha Mhe Bashungwa uongo unaofanana na ukweli.

HATUA: Jana nimefikia hatua ya kumtaka Mhe Waziri aingilie na kuagiza wahusika wachukue hatua, nimewaagiza mawakili wangu wampe DEMAND NOTICE ya siku 14 Waziri achukue hatua hizo, vinginevyo riadha haitakua stable mpaka hili swala liwekwe sawa, otherwise, wanaacha uwezekano wa mambo kama haya kuja kujitokeza tena mbeleni sio tu kwa riadha bali hata kwa michezo mingine kitu ambacho kitailetea taifa aibu miongoni mwa mataifa ya ulimwengu mzima.

HITIMISHO: Ninategemea ndg John Bayo atafanya lolote analoliweza kunifanyia malipizi (retaliation), lakini mimi sina wasiwasi nimeapa kutetea riadha ya leo na hata ya kesho, come what may.

"Kama Watanzania walikuwa wanajiuliza tunakwama wapi? Jibu ndiyo hizo figisu za kubebana bebana hadi kuwaweka wateule wa Rais wa nchi majaribuni"
 
Huyo naye alikuwa anapiga kelele huko kabla hawajampa kauongozi, walipompatia ndio walewale olympic wanariadha na mabondia akina kidunda wakawa wanadundwa tuu
 
Najiuliza ni kwanini Waziri yupo bubu kwa hili swala la Kikatiba? Hapo kuna harufu ya rushwa kubwa, hadi Waziri kimya?
 
Kidunda hahusiki na uongozi wa riadha, Kidunda ni ndondi wapo Olimpiki yao pale kifa mbulahati

Main nimezungumzia wanariadha waliokuwa wanakwenda kuwakilisha nchi kwenye olympic na huyu kidunda enzi hizo alikuwa anacheza ngumi za ridhaa na walikuwa wanaambatana kam timu ya taifa ( riadha +ngumi) na wote waliitia aibu nchi. Hivyo nimejumuisha na ngumi kama OBITER DICTUM na sio RATIO DESIDEND
 
Umeupiga mwingi mpaka unatoka nje
 
Main nimezungumzia wanariadha waliokuwa wanakwenda kuwakilisha nchi kwenye olympic na huyu kidunda enzi hizo alikuwa anacheza ngumi za ridhaa na walikuwa wanaambatana kam timu ya taifa ( riadha +ngumi) na wote waliitia aibu nchi. Hivyo nimejumuisha na ngumi kama OBITER DICTUM na sio RATIO DESIDEND
Duh Mkubwa umeupiga mwingi hadi kisutu...kuna mengi yakufanyika Riadha ikae sawa
 
Back
Top Bottom