Tatizo lenu mna uelewa mdogo,hivi kwanini mridhi wa Rais Uhuru azungumziwe sasa hivi hata hajamaliza kuteua baraza la mawaziri? Huoni media propaganda zimeanza kumpamba Gideon mapema sana ili kuua umaarufu wa Ruto?bro,nimekosea wapi?coz hiyo thread nimeitoa kwenye official media ya kenya.
Ili ugombee urais seriously na kuwa na uwezekano wa kushinda Kenya, sharti!
1. Uwe kabila kubwa, Kikuyu, Kalenjin, Jaluo, Kamba au Luhya.
2. Kabila lako lote liwe nyuma yako, kabila lako ndio mtaji wako wa kuanzia.
Kwa sasa, Kikuyu wapo na Uhuru lakin 2022 mpaka sasa hakuna Mkikuyu anayeonekana wazi kulibeba kabila, Ruto janja janja aliishammaliza Peter Keneth aliyekuwa anaonekana atakuwa nyota ya Wakikuyu. Wengi wa watarajiwa wengine sasa wapo na Ruto.
Kalenjin ambalo ndio kabila la Ruto na Gideon Moi kwa sasa wapo na Ruto, sasa Gideon hawezi kuota urais kabla ya kulikamata kabila.
Kamba wapo na Kalonzo Musyoka na Jaluo kama kawaida wapo chini ya ukoo wa Odinga.Waluhya hawajawai kuwa na muungano dhabiti sana, huku kwa sasa ni eneo pia la Odinga.Odinga akistaafu 2022, kutajipanga upya.Either Mudavadi, Wetangula na Wamalwa rafiki wa Ruto wanaweza kubeba kiasi cha ushawishi.
3. Baada ya mtaji wa kabila lako, ungana na wengine au mwingine mwenye mtaji mzuri wa kabila lake, Uhuru + Ruto au Raila + Kalonzo.
Kuelekea 2020, kila mmojawapo wa magiant wa kabila hizi watajipanga kutengeneza miunganiko ya ushindi, kwa Kikuyu kutokuwa na mbadala wa wazi wa Uhuru mpaka sasa ni faida kwa Ruto,hatujui ya 2020.
Lakin anaweza pia kuja kuungana na Raila, Kalonzo au Alfred Mutua kama ataweza kumpunguza nguvu Kalonzo. Muda utaongea.Gideon so far yupo loose tu. Hana pa kushikiria zaidi ya Baba yake na rafiki wa toka utotoni, Uhuru.Hii bado haitoshi kwa Kenya kuwa mtaji wa uraisi.
Never underestimate hustler William Ruto.Akili yake ipo sharp sana.
How ‘hustler’ Ruto broke into exclusive club to launch career