Jana nilipokea mgeni toka mkoani ambaye toka nikutane nae muda wa saa kumi jioni alikuwa akinywa pombe aina ya konyagi iliyo ndani ya pakiti na alikunywa za kutosha mpaka akalewa kabisa.
Tulipo rudi nyumbani aliniomba maji ili anywe dawa.. nikamuuliza "dawa na pombe ulizo kunywa itakuwaje? akanijibu "haina shida" na nikweli akachana blister na kutoa vidonge viwili vikubwa kidogo ya panadol na kuvinywa na asubuhi akavinywa tena.
Sasa najiuliza ni dawa gani hizi zinazoweza kunywewa na mtu aliyelewa tena konyagi na bila ya kudhurika?