Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Gissima ameyasema hayo Desemba 20,2024 wakati wa Ziara yake akiongozana na Viongozi wengine wa Shirika katika kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme cha Lemuguru kilichopo Mkoani Arusha.
Gissima amesema kituo hicho cha Lemuguru ni muhimu kutokana na kuunganisha mfumo wa Gridi ya Taifa na mifumo mingine ya Gridi ya nchi za ukanda wa Kaskazini Mashariki mwa Afrika( EAPP ).
Muunganiko huu kikanda wa Eastern African Power pool una jumla ya Nchi wanachama 13.
Mbali ya muunganiko wa Gridi ya umeme ya Tanzania na upande wa Kaskazini mashariki mwa Afrika, Gissima amesema Tanzania inaendelea na Mradi utakaounganisha Gridi yetu na mifumo ya Gridi zingine za nchi zilizo Kusini mwa Afrika yaani Southern African Power Pool.
Akielezea faida zitakazopatikana kutokana na Tanzania kushiriki soko la Kikanda la biashara ya umeme kwa kuingia katika muunganiko wa kuuziana na kununua umeme kwa ukanda wa Kaskazini Mashariki (EAPP) na ukanda wa Kusini mwa Afrika (SAPP), Gissima amesema nchi itafaidika kwa kuuza umeme kutokana na uwekezaji mkubwa Serikali inaoufanya katika miradi ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme nchini.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara ya Kikazi ya Menejimenti ya Shirika kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo walianzia katika mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa nguvu ya maji wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).
Imeandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja
TANESCO,MAKAO MAKUU
DODOMA