Mi naomba nichangie kidogo hapo penye bold. Mapenzi ni complex na mapenzi bila pesa inawezakana kabisa. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo
1. Nimeshaona ndoa nyingi sana za watu ambao hali zao za kiuchumi ni za chini sana lakini wanaishi kwa furaha sana
2. Nimeshaona Wanawake wenye uwezo sana wakiwapenda wanaume wasio na hela wasio na mbele wala nyuma na wakaamua kufunga nao ndoa na wangali wanaishi vizuri
3. Nimeona wakaka wengi tu wenye uwezo wakioa wadada toka familia zisizo na uwezo na wakawa na maisha ya furaha sana.
Hivyo nachotaka kuhitimisha, mapenzi huwa hayaangalii sana uwezo na pesa alizonazo mtu, na ndiyo maana kuna watu waliooa/kuolewa na watu wenye uwezo na bado wanatoka nje ya ndoa zao na watu wasio na uwezo.
Ila nakubali kuwa Pesa inasaidia sana kumpata mtu kwa haraka zaidi hata kama hakukupenda, anaweza kujilazimisha na kujiweka karibu na kufake kila kitu mpaka umuone na yeye anakupenda pia. Ila mahusiano ya namna hii huwa hayana maisha marefu.