Giza-lilivyoacha miili ya watu katika tufani la mauti.

Giza-lilivyoacha miili ya watu katika tufani la mauti.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
KHA-KISA GIZA.

1.Hakika kuna machungu,kushuhudia ajali
Eti amepanga Mungu,basi sisi tusijali
Si Leo ni zama tangu,watu wanatupwa mbali
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

2.Giza lazuia nini,tuwaache wafe maji
Waangamie ziwani,kisa ni waokoaji
Hawatoweza gizani,kweli wao wajuaji ?
Kha eti kisa ni giza, twasitisha kuopoa !.

3.Ama alikwisha jua,wote wameshafariki
Kilobaki kuopoa,miili iso na haki
Ndo mana akaamua,iangamie kwa dhiki
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

4.Hivi kama wangekua,wale waandamanaji
Ni nani angezuia,si hakimu wala jaji
Nguvu wangeitumia,hata kama mauaji
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

5.Wataja kutuambia,kwamba mola mpangaji
Hata yaliyotokea,hatukua wajuaji
Na watachotugawia,ni kibakuli cha uji
Kha eti kisa ni giza, twasitisha kuopoa

6.Twakesha kusubiria,kufa kama kumbikumbi
Kisha waje tonyeshea,wakitoa rambirambi
Twashindwaje kuopoa,hata tuwashe utambi
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !

7.Twashindwaje jichanjia,hili la taifa tezi
Kila Mara larudia,huu sasa ni ulezi
Pengine najiwazia,ngoja wavamie wezi
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

8.Tumeambia dunia,sisi wadhaifu wazi
Alologa kajifia,kafara letu si Nazi
Bali kujiamulia,Nani tumshushe ngazi
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

9.Dunia yatushangaa,hivi tulishindwa vipi
Madaraka ni hadaa,sisi tunaweza lipi
Hakika tumezubaa,tukayaweka makapi
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

10.Pole tu tumeingia,tayari yupo gizani
Nani wakutetea,saa yupo hatarini ?
Kumbe tutaangamia,kama panzi wa mwituni
Kha eti kisa ni giza,twasitisha kuopoa !.

SHAIRI -KHA KISA GIZA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Loving this kind of literature..... Fasihi iliyosheni vina, nahau ngeli za kiarifa na mpangilio wenye kuvutia
Kula 5[emoji109][emoji115][emoji123][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]
Nice piece of literature
 
Back
Top Bottom