Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Msemo huu upo hapa kukutia moyo katika maisha yako na jitahidi kuukumbuka mara kwa mara unapokuwa katika nyakati ngumu za maisha (when it gets dark the stars come out)
Msemo mwengine ambao unashahabiana na huo ni "ukiona kiza kinazidi ujue kunapambazuka" huu ni ukweli ulio wazi kabisa pale mambo yanapokuwa magumu sana na kujikuta unakata tamaa basi kuna wepesi au neema ambayo itakujia na inasemwa msaada wa Mungu unapatikana zaidi pale unapokata tamaa
Kwahiyo haijalishi upo katika changamoto ngumu kiasi gani wakati huu ila kumbuka huu msemo giza linapoingia basi nyota huonekana,ntakupitisha katika mifano kadhaa ya watu maarufu ili ujue madhila waliyopitia na kikaja kipindi ambacho nyota zilionekana baada ya kiza kuingia
Na ikiwa wewe ni mtu ambaye unapenda madini ya kubadilisha namna ya kufikiri,kuwa na mitazamo tofauti na kuiona dunia katika namna tofauti basi mimi mwandishi wako ETUGRUL BEY ndio mambo yangu hayo,nyuzi zangu nyingi sio popular kwasababu naamini nyuzi zangu hazipo kwa ajili ya kila mtu bali kwa wale ambao wanataka kufikiria tofauti na kuishi tofauti na kuyaangalia mambo katika mtazamo tofauti,kama ni mpenzi wa haya mambo basi utapoona uzi wangu ufungue hautakosa kitu cha kujifunza
Okay tuendelee na habar yetu, bwana John Stuart Mill huyu alikuwa ni mwanafilosofa mkubwa wa kiingereza na uchumi,mnamo wa miaka ya 1826 alipata ugonjwa mkali wa afya ya akili akiwa na miaka 20 tu. Aliathirika sana kihisia na kupata msongo mkubwa sana wa mawazo na alifikia katika steji ya kujiua,na wakati huo hakukuwa na utaalamu wa kutibu matatizo kama hayo
Lakini baadae ule msemo wa kiza kinapoingia basi nyota huonekana ulikuja kujidhihirisha,akaja kupona na kuja kuwa mwanafilosofa mahiri wa kiingereza na uchumi,hata na wewe ipo siku tambua kwamba kiza kinapoingia basi nyota zitaonekana utakuja kushaini na huenda ipo siku utakuwepo katika land rover festival hahah
Mtu wa pili ambaye ningependa nae tujifunze na kupata matumaini kutoka kwake ni William James ni greatest thinker of all time,mwana filosofa mashuhuri wa Harvad,huyu alipata madhara au aliathirika kutokana na ugonjwa wa psychosomatic na kupata athari katika macho na tumbo akiwa na miaka 23 tu
Alipata msongo wa mawazo mkali sana mpaka ikafikia kipindi alitaka kujiua,na mpaka uone mtu anataka kujiua basi ujue hakika tatizo ni kubwa sana,lakini baadae kiza kilipoingia na nyota zikaonekana na akaja kuwa mmoja wa greatest thinker wa mda wote katika historia akibobea katika filosofi na saikoloji
Mtu wa mwisho ambaye ningependa tumsome leo ana historia kubwa sana katika taifa la marekani ni sababu ya kuundwa United States of America ni Abraham Lincolin. Daktari na mtalaam wa magonjwa ya akili ambaye ni maarufu sana duniani bwana Karl Menninger katika kitabu chake cha "Vital balance" anasema Abraham Lincoln alipatwa mara kwa mara na msongo wa mawazo ambayo ni tatizo la afya ya akili kiasi ambacho alitaka kujiua.
Kuna kipindi shemeji yake Abraham Lincoln kwa mke mpya alisema Abraham alikuwa kichaa,na hasa pale ambapo baada ya matayarisho yote ya harusi yake kufanyika na watu kuwa tayar ukumbini,lakini mwamba hakutokea na akaja kukutwa amekaa chumbani kwake akiwa na hisia za majuto,kukata tamaa na mambo kama hayo
Mwandishi Dale Carnegie ambaye alitumia miaka mitatu kusoma historia ya Abraham na kuandika bioghapher yake, anasema Lincoln alikuwa ni mgonjwa mno wa mwili na akili pia na mara kadhaa alitaka kujiua,na ikafikia kipindi akaandika shairi maalum la kujiua ambalo lilikuja kuchapishwa katika magazeti ya Springfield
Lakini pamoja na changamoto nyingi alizopitia alikuja kuwa raisi wa Marekani ambaye amekuwa na mchango mkubwa sana na ni sababu ya kuwa United States of Amerika,na inasemwa yeye ndio alipigania sana kuwepo kwa usawa na haki na kupambania sana swala kukomesha utumwa,na inasemwa na wataalamu wa mambo huenda ndio sababu ya kuuwawa kwa kupigwa risasi.
Wasomaji wangu hakika siku zote kumbuka kiza kinapoingia basi nyota huonekana,,haijalishi hauna ajira kwa mda gani,hujaoa au kuolewa kwa mda gani,mambo home hayaeleweki,ndugu hampatani lkn kumbuka kuwa GIZA LINAPOINGIA BASI NYOTA HUONEKANA
Ni hayo tu!