Global Publishers wamuomba msamaha Diva, ni baada ya kutunga uwongo kuhusu Zitto

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
KATIKA Gazeti la Amani Toleo Namba 829 la Septemba 11- 17, 2014, kulichapishwa habari ukurasa wa mbele iliyosomeka :

"DIVA: ZITTO NI MUME WANGU.
Ikikolezwa na dondoo ' Adai ni mke anayetambulika kisheria ' na ' Asema hayuko tayari kuachana naye kirahisi,' ambayo uongozi wa gazeti umekusudia kwa nia njema kutoa ukweli juu ya habari hiyo.
Loveness Malinzi ( Diva). Ufafanuzi huu unalenga kumaliza mkanganyiko uliojitokeza hasa baada ya kuwepo kwa madai kutoka kwa mhusika ambaye ni Loveness Malinzi ( Diva ) kuwa hakuzungumza na gazeti kile kilichoandikwa na kwamba alikuwa anazushiwa ; madai haya aliyawasilisha chumba cha habari kwa njia ya simu na sehemu kuyaweka kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.

Kama hilo halitoshi, Diva alikana kuzungumza na mwandishi wa habari hiyo ambapo alisema mazungumzo yao yalihusu mwaliko wa Kipindi cha Global TV Online ambacho kinarushwa na mtandao unaoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers inayomiliki pia Gazeti la Amani na si vinginevyo.

Malalamiko haya ya Diva yalikuja muda mchache baada ya gazeti kutoka likiwa na habari hiyo ambapo jopo la wahariri wa Amani kabla ya kuchapisha habari hiyo walijiaminisha kuwa ni ya kweli kutokana na taarifa pamoja na vielelezo vya rekodi ya sauti ya mazungumzo alivyoviwasilisha mwandishi kwenye dawati kuthibitisha kuwa alifanya mazungumzo na mhusika kuhusiana na msingi wa habari nzima iliyoandikwa.

Mheshimiwa Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Kama tulivyoeleza, baada ya habari hiyo kutoka na kipande cha sauti kuingizwa kwenye Tovuti ya Global Publishers, ndipo yalipoibuka madai hayo huku baadhi ya wasomaji wakieleza kuwa ile siyo sauti ya Diva, hapo ndipo uongozi wa gazeti ulipoamua kufuatilia ukweli na kubaini yafuatayo.

Pamoja na ukweli kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe ( Mbunge wa Kigoma Kaskazini ) na Diva wana ukaribu , mazungumzo kati ya mwandishi na mwanadada huyo kuhusiana na kauli yake ya : "Zitto ni Mume Wangu, " hayakufanyika na kwamba mwandishi alipika habari na kutengeneza sauti ya Diva kwa lengo la kuwahadaa wahariri kwa nia mbaya.

Kwa msingi huo sisi kama chombo cha habari makini, kinachosimamia weledi, kulinda na kuheshimu haki za binadamu; tunachukuwa nafasi hii kumuomba radhi Diva, Mheshimiwa Zitto, sanjari na jamii kwa ujumla kwa usumbufu wowote uliosababishwa na habari hiyo.

Aidha uongozi unapenda kuutangazia umma kuwa, hatua kali za kinidhamu zimeshachukuliwa dhidi ya mwandishi husika sambamba na onyo kwa viongozi wote wa gazeti kwa udhaifu uliojitokeza katika habari hiyo.

Tunaomba jamii ielewe kwamba Global Publishers siku zote inasimamia UKWELI na kamwe hairuhusu kabisa habari za uongo kuandikwa katika magazeti yake.

Jamii iendelee kutuamini na kushirikiana nasi katika kusimamia weledi wa uandishi wa habari.

Milango ya kukosolewa iko wazi, hivyo kwa mwenye malalamiko yoyote juu ya habari zetu, iwe ni uongo au kutotendewa haki, asisite kuwasiliana na viongozi kwa hatua zaidi.

Ndimi Mhariri Kiongozi, Magazeti Pendwa.
 

Attachments

  • 1411014674615.jpg
    59.8 KB · Views: 781
Kwa hiyo kwa wale ambao hawalalamiki yanakua ni kweli au naomba tueleweshane katika hili
 
Kwa hiyo kwa wale ambao hawalalamiki yanakua ni kweli au naomba tueleweshane katika hili

Wenyew walikuwa na ushahidi wa clip ya audio ya diva aliyokuwa akizumgumza kuwa ni kweli aliyoyasema kwenye gazeti, ila hata mimi nilisikia hiyo clip, ile sio sauti ya diva hata kidgo wametengeneza tu, watu ndo wakawaponda gpl kuwa wazushi na ni kweli diva hajaongea na magazeti kuhusu zito bali ni wao walitunga ndo maana wanaomba msamaha
 

Ile sauti haikua ya Diva hata kidogo.........

Global wamezidi habari za uongo hata kama ni kutafuta pesa wamezidi duh
 
Ile sauti haikua ya Diva hata kidogo.........

Global wamezidi habari za uongo hata kama ni kutafuta pesa wamezidi duh

Ni uwongo mtupu, hata ambao hawampendi diva kwa hili walimtetea maana ni uwongo wa hali ya juu, kumbe maskini hata hausiki na ile habari diva wa watu, ila global na wenyew kiboko wametunga kila kitu, wana jiamini
 
Ni uwongo mtupu, hata ambao hawampendi diva kwa hili walimtetea maana ni uwongo wa hali ya juu, kumbe maskini hata hausiki na ile habari diva wa watu, ila global na wenyew kiboko wametunga kila kitu, wana jiamini


mi nasomaga Heading ile nilivyoiona nikataka kujua zaidi kufungua

sauti ninayokutana nao looh..... hata kama anapendaga kick ila hili lilizidi
 
mi nasomaga Heading ile nilivyoiona nikataka kujua zaidi kufungua

sauti ninayokutana nao looh..... hata kama anapendaga kick ila hili lilizidi

Eti na wenyew wanasema kuna mtu aliwapa hiyo clip ya diva na wenyewe hawakujua kama sio yake, kweli ile sauti ya diva? Hii haingii akilini hata kidogo, aya achilia mbali sauti, kwa nini wadanganye umma kuwa diva alisema vile wakati sio kweli? Na wala hawakumpigia simu, maana hadi diva alishangaa ila mi nikajua anajishaua kumbe kweli diva hajui chochote , hawa akina mnaly na mussa mateja na demu wao imelda soon kibarua kitaota nyasi, maana apa issue sio sauti ya diva ila ni kuuongopea umma kuwa diva kasema zitto ni mume wake wakati hajasema hata
 

kwakwli wameidanganya jamii aisee........
na pale walivyojifanya mwandishi alimpigia sim na kuongea nae YAMEWASHUKA leo

Imelda Cheusi dawa nae kwa umbea anajitahidi
 
kwakwli wameidanganya jamii aisee........
na pale walivyojifanya mwandishi alimpigia sim na kuongea nae YAMEWASHUKA leo

Imelda Cheusi dawa nae kwa umbea anajitahidi

Mimi hiyo michezo yao sijui ya kuwa waliongea na msanii akawakibu vile sijui simu iliita bila kupokelewa ni uwongo mtupu, wanaonaje aibu sasa,

Na mimi naona wameomba msamaha kwa sababu ya mh. Zitto, maana walimchafua sana yeye na sio diva, maana diva kama aliweza kujitangaza kutembea na zitto sidhan kama ni mzima kichwani na ndio maana ilikuwa rahis watu kuamini kuwa yale maneno kwel kasema diva , hawa jamaa wanajua sana kucheza na akili za watu
 
Diva nahisi kaachwa na GK maana siku hizi zile clip za kuangua mapera haweki tena insta....ana kazi ya kusifia wanaume wengine tuu
 
Diva nahisi kaachwa na GK maana siku hizi zile clip za kuangua mapera haweki tena insta....ana kazi ya kusifia wanaume wengine tuu

Na yale maneno aliyokuwa anaongea kuhusu zitto, lazima apigwe chini, yule demu hamnazo kabisa
 
Na yale maneno aliyokuwa anaongea kuhusu zitto, lazima apigwe chini, yule demu hamnazo kabisa

Kuna siku ndugu yake (diva) mtoto wa malinzi anaitwa jamimah alicomment kwenye post ya diva kua hajui zitto kampa nini ndugu yake (diva) maana anampenda hatari...nilishangaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…