Go Out and Sell Yourself-Nenda Kajiuze

Go Out and Sell Yourself-Nenda Kajiuze

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Katika safari ya ujasiriamali huwa kuna changamoto nyingi sana lakini kubwa kuliko ni namna ya kupata wateja.

Unaweza kuwa na Bonge la Idea lakini bado usipate wateja,Unaweza kuwa na Product nzuri sana lakini usipate wateja na Unaweza kuwa na soko zuri sana lakini bado usipate wateja,Unaweza kuwa na kila kitu "By the Book" na bado usipate wateja.

Cha kushangaza zaidi ni hiki,Unaweza kuwa huna idea ya maana wala huna product ya maana wala huna soko wala huna locationa bomba lakini ukiwa unauza kupita kiasi.Swali inakuaje iwe hivi?
Tofauti iko katika namna unavyojiuza,"People do not buy your idea/product/location-People buy into you""To sell your self you must put yourself up for sale,you must have the message clearly on your forehead that you are up for sale"

Nimeweke kizungu hapo maana kuna watu wanaamini Point lazima iwekwe kwa kizungu ila Ninachotaka kusema ni kwamba watu hawanunui bidhaa,wala wazo,wala location bali wanakununua wewe,Kama wewe hujiuzi basi hawawezi nunua chochote chako.

Ukitaka kufahamu ukweli wa hilo angalia mabadiliko yanayotokea katika biashara ya Bar ukibadilisha wahudumu na kuleta wahaudumu wapya na wasafi,Angalia mabadiliko yanayotokea katika biashara yako ukiweka binti wa kike mrembo na mkarimu.Simaanishi kwamba biashara ili iuze lazima uweke mwanamke au bar ili iuze lazima uweke wahudumu warembo(Uzuri unategemea na muonaji) Hapana namaanisha kwamba watu hununua zaidi ya kile unachouza na wako tayari kulipia zaidi kama wakiona thamani ya pesa.

Kujiuza ni rahisi kusema ila sio rahisi kutekeleza.Ni hatua ambayo inahitaji ujielewe,uelewe wateja wako na zaidi uwe tayari kubadilika na soko na kusikiliza yale yanayosemwa n a yasiyosemwa.

Tujdili hapa mbinu unaweza tumia katika kujiuza ili kufikia malengo yako ya kibiashara na kimaisha

Karibuni
 
Ujumbe uko murua sana ubarikiwe

Je kujiuza kuna uhusiano wowote na personal branding !?
SIpendi kutumia neno personal branding maana liko artificial sana.Ili yanalandana.Personal Branding ina maana ya kuwa na Professiona/Public image tofauti na True Personal trait.
 
Mie nimepractice sana biashara...kubwa na ndogo! Hadi sasa niko na somo moja tu! Uaminifu!

Mjasiriamali usiwe mtu wa kona kona...hakikisha mteja ameridhika na bidhaa yako..asiporidhika msikilize shida yake ikiwezekan nxt tym mpromis utampa offer au kadiscount! Ukiwa mwaminifu , mchangamfu na usiye na lugha za kukera unafika mbali
 
Back
Top Bottom