kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Huu ni mda wetu kuonyesha Afrika uwezo wetu na nguvu zetu. Daima tumekuwa chini kwa kipindi kirefu lakini muda huu ni wakati wetu. Mshindi siku zote huwa hana thamani mbele ya wapinzani wake, kila mtu huwa ana mashaka juu yake.
Lakini Mungu akisema ndiyo ni ndiyo hata kama unatumia nini kupata ushindi wako, Mungu atakubariki kwa kile unachotegemea kukupa ushindi hata kama ni hirizi. Mungu atalipa uwezo na nguvu zaidi kwasababu muda wako wa kufanikiwa umefika.
Watu wengi watasema kwanini unamuweka Mungu katika mambo yako ya mpira, rafiki zangu ngoja niwaambie kitu, kila unachokifanya hapa duniani kiwe kibaya au kizuri Mungu anakibariki. Na nasema nikiona Young Africans inaenda hatua ya makundi, kaka zangu mniamini Young Africa itafika mbali kuliko klabu yoyote Tanzania.
Wote tusome andiko hili na tuombe kwasababu ya timu yetu pendwa, hakuna kinachoshindikana.
"Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia."
Malizia "Eeh Mungu naweka Yanga mikononi mwako naamini huu ndiyo muda wetu. Rehema na baraka zako ziwe juu ya timu hii", na sisi wote tuseme amen.
Hii ni picha ya Mazembe wakiwa kanisani kabla ya mechi yao na Vipers Uganda, na huku ndiyo kuna siri ya ushindi. View attachment 2387867
Yule admin wa "Young group what" njoo uchukue hii, kila mwana Yanga apige dua hilo, naamini kwa uwezo wake aliye juu lazima tutatoboa tu.