Godbless Lema, mmoja wa Wanasiasa wa chama cha upinzani CHADEMA, ameongea kwa ujasiri kuhusu Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akimtaka akatae vikali kuitwa "Alfa na Omega".
"Nilisema mimi namheshimu Mwenyekiti (Mbowe), ni kaka yangu na nikataka jambo hili alichukue kama sanaa ya demokrasia, nimemuangalia Azam TV, Mwenyekiti wetu anasema....kwanza kuna kitu kitoke kwenye fikra yake, namuomba akitoe yeye mwenyewe haraka sana, kwanza akatae mara moja haraka iwezekanavyo kuitwa Alfa na Omega, Mwenyekiti sisi hawezi kuwa Alfa na Omega yeye sio Mwenyezi Mungu"