SI KWELI Godbless Lema asema mgogoro wa Ngorongoro umepandikizwa na wafanyabiashara wa utalii kutoka Kenya

SI KWELI Godbless Lema asema mgogoro wa Ngorongoro umepandikizwa na wafanyabiashara wa utalii kutoka Kenya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Godbles Lema awachana wamasai, amesema ana taarifa kuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wa Kenya. Nimependa sana ujasiri wa Lema, kuwa mpinzani siyo kukataa kila kitu.

Suala la Ngorongoro limeileta nchi pamoja, hata wapinzani wameungana na Serikali.

GODBLESS LEMA.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na taarifa inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na Mbunge wa zamani wa Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema akisema kinachoendelea Ngorongoro hivi sasa kimechochewa na wafanyabiashara wa Kenya.

"Nimepokea simu toka kwa Ole Lankenua wa Kenya amenihakikishia kuwa hili suala la Ngorongoro limepandikizwa na baadhi jamii ya wafanyabiashara wa utalii kenya wenye ndugu Tanzania. Tukiendelea na kelele hizi tunawanufaisha zaidi majirani kuliko sisi. Arusha na utalii zilindwe" unasema ujumbe huo uliohifadhiwa hapa.

Taarifa hii inasambaa kipindi ambacho Serikali imetoa amri rasmi ya kufuta vijiji vya Ngorongoro kupitia tangazo la Serikali namba 673 la Agosti 2, 2024 huku wakazi hao wakionesha kutokuridhishwa na jambo hilo.

Taarifa hii imetolewa na Godbless Lema?
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hii iliyochapishwa kwenye mtandao wa X Agosti 18, 2024 na kubaini haikutolewa na Godbless Lema kama inavyodaiwa.

Kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia maneno muhimu yanayopatikana kwenye ujumbe huo, JamiiCheck haijapata kumbukumbu zozote zinazoonesha ulichapishwa na Lema.

Aidha, Agosti 19, 2024, Lema alikanusha ujumbe huo aliouita wa kutengenezwa na kubainisha kuwa yupo pamoja na jamii ya wamasai kwenye madhira wanayopitia.

"Puuzeni UPUMBAVU na PROPAGANDA za Chawa na Kungunizi. Ujumbe hapo chini sio wangu bali ni Photoshop. Mimi niko na Jamii ya Wamasai inayoteswa na kunyanyaswa na serikali yao. Sijapokea simu kwa mtu yoyote kutoka Kenya ktk sakata hili. jamii ya watu wa MAASAI wana hadhi/heshima kuliko wanyama. Madai yao yazingatiwe. Mkianza hivi mtakimbia. Trust me , we also know stupid things , lakini tunajali hekima na busara zaidi" aliandika Lema kwenye ujumbe uliohifadhiwa hapa.

Awali, Agosti 3, 2024, jamii ya wamasai ilitoa tamko kupinga kunyang'anywa haki ya kupiga kura uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kutokana na kuhamishwa kwa majina yao kwenye dafrari la kudumu la wapiga kura.
Asanteni sana JamiCheck kwa kuhakiki na kunipa majibu ya uhakika.
 
Duh,
Kwamba siyo Lema, bali ni janjajanja na kutapatapa kwa chawa wa mama!!!
 
Back
Top Bottom