Godbless Lema awapa onyo zito CHADEMA kuelekea Uchaguzi mkuu wa 2025. Akiri CCM kufuatilia Uchaguzi wao wa ndani

Godbless Lema awapa onyo zito CHADEMA kuelekea Uchaguzi mkuu wa 2025. Akiri CCM kufuatilia Uchaguzi wao wa ndani

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kufikia hvi sasa bado, Godbless Lema hajaainisha anamuunga mkono nani kati ya Lissu ama Mbowe.

Na wakati watu wanasubiri atoe msimamo wake, Lema ametoa onyo zito kwa baadhi ya makada wa CHADEMA Kutokana na kauli ambazo wanazitoa.

============================================

photo_2024-12-29_15-24-41.jpg

CCM wanatufuatilia sana, wana hifadhi kila kauli zetu juu ya wagombea wetu wote ktk mchakato wa uchaguzi wa Chama wa viongozi wakuu Mwezi January , bila shaka watazitumia kauli hizi Mwaka 2025 kama tutashiriki na kutakuwepo na uchaguzi huru.

Lakini pia wananchi wana share kila habari inayoleta fitina na uchungu miongoni mwetu. Hii ni hatari. Chama cha siasa za upinzani na harakati za kutafuta utawala bora zinaongozwa na inner purpose na passion, kusudi likifa Chama kinakufa kwa sababu 99% ya viongozi na wanachama wanafanya wajibu wa kazi za Chama kwa kujitolea , sasa watawezaje kujitolea kama hakuna purpose ?

Moral inajengwa na nidhamu . Kwa hali ilivyo sasa tuna uchungu sisi kwa sisi kuliko tulivyo na uchungu dhidi ya CCM , kampeni ya sasa ya dhihaka na matusi kwa viongozi na wananchi ambao hatuwaungi mkono imekuwa kali kuliko kampeni ya kukomesha mauaji na utekaji Nchini.

Let’s get back to the purpose na kila mtu aheshimiwe na kuthaminiwa kwa upande aliouchagua kwa maana ndiyo demokrasi yenyewe.
 
LEMA yupo sahihi, anaumia sana na chama na haridhishwi na situation ya chama ilivyo. Lissu na washabika ndio chimbuko la matatizo yote.
 
LEMA yupo sahihi, anaumia sana na chama na haridhishwi na situation ya chama ilivyo. Lissu na washabika ndio chimbuko la matatizo yote.
Tatizo ni Mbowe kuwa sultani, alitakiwa awe amesoma alama za nyakati siku nyingi.
Wanachama wa kawaida hawana imani naye kabisa wanamuona yupo upande wa watesi wao.
 
Tatizo ni Mbowe kuwa sultani, alitakiwa awe amesoma alama za nyakati siku nyingi.
Wanachama wa kawaida hawana imani naye kabisa wanamuona yupo upande wa watesi wao.

musisingizie wananchi wakawaida, Team Lissu ndio wanaomchafua na kuwaaminisha wananchi wa kawaida kuwa anatumiwa na CCM.
 
Back
Top Bottom