Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini Godbless amesema "ameona juzi kuna mbunge ndani ya Bunge ametaka Bunge lijadili masuala ya watu kupotea na kutekwa, spika anazuia mjadala wa watu kutekwa, lile halina uhalisia wa bunge.
Huwezi kuwa na bunge ambalo mbunge anataka mjadala wa watu wanaopotea na siyo kwamba hakuna. Tumeona kwenye vyombo vya habari kuna mahali kwa mganga wa kienyeji zimekutwa maiti na nimesikia tena zimekutwa Dodoma, kila mahali kuna kilio cha watu kupotea, mbunge anasema ninaomba tujadili hili suala tujue kama ni uzembe wa polisi, au ni vyombo vingine vya ulinzi na usalama, na suala halijadiliwi.
Aidha amesema Watanzania mkiendelea na hii hali na msingi huu wa mawazo mlionao, ya kwamba mpira kwenu una maana, wa Simba na Yanga kuliko maisha ya wenzenu, hii ni nchi ya ajabu. Na mimi ningekuwa na uwezo wa kumuomba Mungu aue Simba na Yanga zisiwepo nchi hii ningeshukuru sana.
"Ni dhahiri kwamba kila mtu atakufa, lakini siyo kufa kwa kutekwa, siyo kufa kwa kuonewa, siyo kufa kwa kupigwa risasi, siyo kufa kwa kudhalilishwa. Kwa hiyo kama kuna jambo la msingi kabisa ambalo serikali inapaswa kulitilia maanani ni kuacha kila kitu, ni pale mtu mmoja anapokuwa katika mashaka ya kupotea au ya kufa, serikali hasa jeshi la polisi, usalama wa taifa ikiwezekana na jeshi la wananchi wanapaswa kuacha kila kitu, watafute nafsi ya mtu mmoja. Israel ukishika maiti yao moja, jeshi lao litaingia vitani kuja kutafuta maiti, ninaomba nirudie mataifa yaliyoendelea huwa yanakwenda vitani kukomboa maiti na ndiyo maana uzalendo unajengwa
Anaitwa GIDEON MLOKOZI MASHANKARA ana umri wa miaka 30, mkazi wa Tabata Segerea, Kazi yake ni mfanyabiashara wa kuuza magari lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa. Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa...
Wanataka tufuatilie siasa zao na tuwe viongozi wa kuwafuata,yaani tunavyohangaika na simba na yanga ndivyo tuhangaike na mashudu yao,baada ya uchaguzi ujao watafute kazi ya kufanya
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini Godbless amesema "ameona juzi kuna mbunge ndani ya Bunge ametaka Bunge lijadili masuala ya watu kupotea na kutekwa, spika anazuia mjadala wa watu kutekwa, lile halina uhalisia wa bunge.
Huwezi kuwa na bunge ambalo mbunge anataka mjadala wa watu wanaopotea na siyo kwamba hakuna. Tumeona kwenye vyombo vya habari kuna mahali kwa mganga wa kienyeji zimekutwa maiti na nimesikia tena zimekutwa Dodoma, kila mahali kuna kilio cha watu kupotea, mbunge anasema ninaomba tujadili hili suala tujue kama ni uzembe wa polisi, au ni vyombo vingine vya ulinzi na usalama, na suala halijadiliwi.
Aidha amesema Watanzania mkiendelea na hii hali na msingi huu wa mawazo mlionao, ya kwamba mpira kwenu una maana, wa Simba na Yanga kuliko maisha ya wenzenu, hii ni nchi ya ajabu. Na mimi ningekuwa na uwezo wa kumuomba Mungu aue Simba na Yanga zisiwepo nchi hii ningeshukuru sana.
"Ni dhahiri kwamba kila mtu atakufa, lakini siyo kufa kwa kutekwa, siyo kufa kwa kuonewa, siyo kufa kwa kupigwa risasi, siyo kufa kwa kudhalilishwa. Kwa hiyo kama kuna jambo la msingi kabisa ambalo serikali inapaswa kulitilia maanani ni kuacha kila kitu, ni pale mtu mmoja anapokuwa katika mashaka ya kupotea au ya kufa, serikali hasa jeshi la polisi, usalama wa taifa ikiwezekana na jeshi la wananchi wanapaswa kuacha kila kitu, watafute nafsi ya mtu mmoja. Israel ukishika maiti yao moja, jeshi lao litaingia vitani kuja kutafuta maiti, ninaomba nirudie mataifa yaliyoendelea huwa yanakwenda vitani kukomboa maiti na ndiyo maana uzalendo unajengwa
Tusipojua tatizo letu haswa ni lipi tutamlaumu kila mtu anayekatiza mbele ya macho yetu.
Simba na Yanga kwa miaka mingi hazikuwahi kuwa na ukubwa wenye kulingana na majina yao. Walifanana na Simba aliyeloweshwa na maji ya mvua, wakaishia kujikunyata.
Hivi sasa wanaanza kuishi kadri ya ukubwa halisi walionao na kusema ukweli safari ya wao kuwa wakubwa zaidi bado haijafika hata nusu.