Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amezitaka Halmashauri ya Jiji la Arusha na taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kusafisha mitaro iliyoziba kwa taka na kuondoa vizuizi vinavyoweza kuzuia mtiririko wa maji ya mvua.
Hizi ni sehemu chache tu za mitaro ya Jiji la Arusha. Mingine imejaa taka, mingine imeziba, na mingine inatumika kuhifadhi nguzo za TANESCO. Huu ni upuuzi wa kiutendaji unaohitaji maelezo na hatua za haraka kutoka kwa mamlaka zinazohusika.
Wakati TMA ikitoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mvua kubwa zinazohusishwa na El Niño, Halmashauri ya Jiji la Arusha na taasisi nyingine zinazohusika zinafanya nini ?Mnasubiri mvua zianze kuharibu nyumba, biashara na mali za wananchi ndipo muanze kuamka?
Mitaro ni miundombinu ya kuzuia maji ya mvua yasilete maafa, si dampo la taka wala ghala la kuhifadhi nguzo. TANESCO nayo inapaswa kueleza kwa nini nguzo zake zimehifadhiwa kwenye mitaro hiyo na kuhakikisha hazizuii mtiririko wa maji.
Inasikitisha kuona maandalizi ya kuzuia maafa yakionekana kupuuzwa, ilhali gharama za uzembe huu zitalipwa na wananchi wasio na hatia.
Ninakemea vikali hali hii na kuzitaka mamlaka zinazohusika ziamke kutoka kwenye usingizi wa kiutendaji. Safisheni mitaro, ondoeni vizuizi, kagueni mifumo yote ya kupitisha maji na wekeni wazi hatua mnazochukua.
Wananchi hawahitaji visingizio baada ya maafa, wanahitaji hatua kabla ya maafa.
ARUSHA HAIHITAJI MATAMKO YA BAADA YA MAFURIKO. INAHITAJI UWAJIBIKAJI SASA!
Katika hoja zilizotolewa na Raia huyo Nami pia nimeona ni muhimu kuchangia Kwa hoja kwamba, Takribani Bilioni 730 zimetendwa Kwa kuzibiti na kusaidia El Nino kutoathili watu na Mali zao huku miundombinu wezeshi ikiendelea kuwa mibovu, swali ni
Je Gharama zilizotengwa na Serikali ni Kwa Maslahi ya Nani au huu Ndio ufusadi, ubadhirifu wa Mali ya Umma na Uzembe wa Mamlaka husika.?
TANESCO na Mamlaka nyinginezo za Mazingira Kote Tanzania nzima Mnapaswa kuchukuwa hatua kwenye hili.