Godbless Lema: Wakati nakesha club house kuchangisha michango, Wenje alikuwa Canada akipiga picha kwenye madaraja

Godbless Lema: Wakati nakesha club house kuchangisha michango, Wenje alikuwa Canada akipiga picha kwenye madaraja

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kumbe wakati Lema anachangisha pesa za Join The Chain, Wenje alikuwa bize na utalii?

Siku ya leo Godbless Lema akizungumza na wanahabari kuhusu a tuhuma zilizotolewa na Ezekia Wenje, Mgombea wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara na Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Victoria amesema:


"Mimi nilikuwa ninakesha kwenye mitandao ya kijamii kama Clubhouse kukusanya pesa kwa ajili ya Join the Chain, kwasababu Australia wakiamka inabidi niwe Clubhouse kuhamasisha, Australia wakilala na Japan wakiamka lazima niwe kwenye Clubhouse.

Huyu Wenje tulikuwa naye huko Canada labda kazi yake ilikuwa ni kupiga picha kwenye madaraja, kwasababu hajawahi kushughulika na kazi yoyote ya kimataifa ya kusaidia chama hiki.

"Ule mtandao nilioutengeneza wa kukusanya pesa ndani na nje ya nchi ukaanza kufanya kazi moja ya msingi sana, wakati Mwenyekiti Mbowe alipokuwa jela, ikabidi Tundu Lissu awe anasafirishwa kwenda Ujerumani na kwingine kuongea wahisani wa kimataifa kwa ajili ya kuweka shinikizo Mwenyekiti atoke gerezani

Lakini huyu Wenje nimesikia anasema kwamba hawa watu walikuwa wanakusanya pesa ya Join the Chain kumfanyia mapinduzi Lissu awe Mwenyekiti badala ya Mbowe. Kimsingi mtandao wetu ulimsaidia hata Lissu kuwezesha Mwenyekiti atoke"

Lema Wenje.png

Source: Jambo TV Online

Tazama pia: Ezekiel Wenje: Kuhusu zilipoenda pesa za Join The Chain muulizeni Godbless Lema. Yeye ndo alikuwa Mwenyekiti!
 
Lema kaongea ya moyoni..lema ni big brain 🧠 "Think tank" amesema ukiwa na detarmination unaweza ukauza VITUMBUA/ VITAFUNIO Na unaweza kufanikiwa kimaishaa..

Kamwita WENJE Boya...pia lema kaongea kweli tupu kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania..kaonyesha/ weledi/ upeo kupevuka kwa Hali ya juu.

All in all,
Ni mwendawazimu pekee anae weza kuamini team mbowe na watu aina mjaluo ojwang a.k.a WENJE ni muda Sasa chadema I be restored
 
Chama cha mipasho na mambo ya kitoto kesho wenje ataita press ya kujibu upuuzi nani anafadhili hizo press mahotelini!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Afu Mwenyekiti wako alivyotoka Gelezani kaanza kuchangisha ukasusa - sasa kwa taarifa yako alijua hukuwa na lengo jema.
 
Back
Top Bottom