Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 14,578
- 31,662
- Thread starter
-
- #381
Watu wanaona contradictions zipo kabisa lakini wanaamua tu kukaza fuvu. Kuendelea kutetea imani zao walizo aminishwa.Nahitaji kufikia kiwango gani cha uelewa ili niweze kuelewa jinsi Mungu anayeelezwa kuwa na Upendo usio na kifani, mwenye uwezo wote na mamlaka yote, anaweza kuruhusu mabilioni ya watu kupoteza maisha wakubwa kwa wadogo kutokana na majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano, na magonjwa hatari kama Ebola?
Ikiwa Mungu ni mwenye upendo mkamilifu, kwa nini ulimwengu umejengwa kwa namna ambayo sheria zake za kimaumbile husababisha maafa makubwa yanayogusa hata wasio na hatia? Je, ni aina gani ya mpango au hekima inayoweza kuhalalisha mateso ya mtoto anayekufa kwa ugonjwa au familia inayofutwa na tetemeko la ardhi?
Zaidi ya hapo, leo hii nchini Tanzania na katika nchi nyingi za Afrika, wapo watu wenye albinism wanaoishi katika mateso ya kudumu kutokana na miale ya jua inayochubua ngozi zao kwa sababu ya ukosefu wa melanin. Kama Mungu ni mwenye huruma na uwezo wa kuzuia hali hiyo, kwa nini aliruhusu wazaliwe katika mazingira ambayo miili yao haiwezi kustahimili hali ya kawaida ya mazingira?
Na si watu wenye albinism pekee. Kuna watu wengi huzaliwa na matatizo mazito ya kibaolojia, kasoro za kinasaba, ulemavu wa viungo, au magonjwa sugu hali ambazo, kwa mujibu wa imani ya Mungu mwenye uwezo wote, zingeweza kuzuiwa kabla ya kuzaliwa kwao.
Hoja hii si mpya. Charles Darwin aliwahi kuandika kuhusu nyigu aina ya Ichneumonidae (ichneumon wasp) ambao hutaga mayai ndani ya mwili wa mdudu-hai; watoto wa ichnemonidae hula mwili wa mwenyeji polepole (mdudu-hai) hadi afe. Darwin aliona ugumu wa kuoanisha ukatili huu wa kimaumbile na wazo la Mungu mwenye huruma kamili. Alisema hangeweza kushawishika kwamba Mungu mwenye rehema angeumba mfumo wa namna hiyo kwa makusudi.
Aidha, ni muhimu kufafanua msimamo wa wasioamini Mungu (atheists). Wengi wao hawadai kutokuamini kwa sababu tu “hawamwelewi Mungu anayefanya kazi beyond human comprehension.” Badala yake, wanadai kutumia njia zilezile zinazotumiwa na waumini wanapojaribu kumuelewa Mung, kuuliza maswali, kuchambua maandiko, kutafakari hoja za kifalsafa, na kutafuta ushahidi.
Wanapouliza maswali magumu ambayo kwa karne nyingi hayajapatiwa majibu yanayokubalika kwa wote, kuhusu uovu wa asili, na wanapoomba uthibitisho wa uwepo wa Mungu kama Allah, Mungu wa Utatu (Trinitarian God), au Yahweh, lakini hawapati ushahidi wa kimajaribio au wa kimantiki unaowaridhisha, wao huchagua kutokuamini.
Kwao, tatizo si kukataa kitu wanachokielewa; bali ni kutokushawishika na hoja au ushahidi uliopo. Kwa mantiki yao, kama madai ni makubwa, Mungu mwenye uwezo wote, mwenye kujua yote, na mwenye upendo kamili, basi kiwango cha uthibitisho kinapaswa kuwa kikubwa sawasawa na madai hayo.
Hivyo basi, swali la msingi linabaki:
Je, tatizo liko katika mipaka ya uelewa wa kibinadamu, au kuna mvutano wa kimsingi kati ya dhana ya Mungu mwenye upendo mkamilifu na uhalisia wa mateso makubwa yasiyochaguliwa na binadamu?
View: https://www.instagram.com/p/DUnBv60jcLP/?igsh=MWV5bjFtbGl2YnYxYQ==
Kwa kutunia mfano wa kisa hicho hapo juu , nieleweshe test hapo imeenda kwa nani nk.
Mabishano mmeyataka wenyewe Mungu ameweka kila kitu wazi kwenye vitabu vitakatifu ,wewe unafeli wapi mkuuMungu angekuwa anajitetea mwenyewe wala kusingekuwaga na mabishano ya kidini.
Kusingekuwa na mabishano kati ya Allah vs Jesus.
Kusingekuwaga na mabishano kati ya wakristo na waislamu.
Mungu angefahamika yupo bila utata au utofauti wa kiimani.
Wala kusingehitajika imani ya kuamini uwepo wa Mungu.
Kila mtu angejua kwa uhakika kabisa Mungu yupo bila kuhitaji imani yoyote ile.
Hizi imani za Ukristo, Uislam, uhindu, ubudha ndio zinaleta mabishano baina ya watu duniani. Na hii ni wazi kabisa Mungu hayupo kujitetea mwenyewe.
Ndio maana mabishano baina ya waamini hayaishi.
🤣🤣Mtumishi ata ww ongea na huyu mtu wako😹
nakusaidia wewe usitumbukie shimoniKama Mungu hahitaji wewe umtetee mbona unahangaika kuandika hapa kumtetea uwepo wake?
Si uache huyo Mungu ajitetee mwenyewe kama ana huo uwezo?
Hakuna haja ya wewe kuandika paragraph ndefu kunijibu ikiwa huyo Mungu yupo kujijibia mwenyewe.
Huyo Mungu kama yupo, ajitetee mwenyewe na kujibu haya maswali yangu.
Mi nimekupa case study uitumie, wewe umeiweka pembeni case study ya kujifunziaMkuu, Qur’an iko wazi kwamba mtihani ni kwa binadamu, si kwa Mungu.
Qur'an 67:2 — Mungu ameumba mauti na uzima ili awajaribu ni nani bora kwa matendo.
21:35 — Tunajaribiwa kwa mazuri na mabaya.
2:155 — Hofu, njaa na upungufu ni sehemu ya mtihani.
Mtihani unaenda kwa nani? Kwetu sisi.
Si ili Mungu ajue (Yeye tayari anajua), bali ili uchaguzi wetu ujidhihirishe kwa vitendo na tuwajibike.
Kama hakuna test, basi hakuna tofauti ya mwenye kufanya maovu na anayejizuia — na hapo haki inakosa maana.
Uislamu unasimama hapo: Mungu anajua, lakini mwanadamu anachagua — na kwa uchaguzi wake anapimwa.
Mi nimekupa case study uitumie, wewe umeiweka pembeni case study ya kujifunzia
Hapo nani kapewa test, hao watoto, mama yao, baba yao, majirani ? Jamii? au alowanyonga?
Nahitaji kufikia kiwango gani cha uelewa ili niweze kuelewa jinsi Mungu anayeelezwa kuwa na Upendo usio na kifani, mwenye uwezo wote na mamlaka yote, anaweza kuruhusu mabilioni ya watu kupoteza maisha wakubwa kwa wadogo kutokana na majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano, na magonjwa hatari kama Ebola?
Ikiwa Mungu ni mwenye upendo mkamilifu, kwa nini ulimwengu umejengwa kwa namna ambayo sheria zake za kimaumbile husababisha maafa makubwa yanayogusa hata wasio na hatia? Je, ni aina gani ya mpango au hekima inayoweza kuhalalisha mateso ya mtoto anayekufa kwa ugonjwa au familia inayofutwa na tetemeko la ardhi?
Zaidi ya hapo, leo hii nchini Tanzania na katika nchi nyingi za Afrika, wapo watu wenye albinism wanaoishi katika mateso ya kudumu kutokana na miale ya jua inayochubua ngozi zao kwa sababu ya ukosefu wa melanin. Kama Mungu ni mwenye huruma na uwezo wa kuzuia hali hiyo, kwa nini aliruhusu wazaliwe katika mazingira ambayo miili yao haiwezi kustahimili hali ya kawaida ya mazingira?
Na si watu wenye albinism pekee. Kuna watu wengi huzaliwa na matatizo mazito ya kibaolojia, kasoro za kinasaba, ulemavu wa viungo, au magonjwa sugu hali ambazo, kwa mujibu wa imani ya Mungu mwenye uwezo wote, zingeweza kuzuiwa kabla ya kuzaliwa kwao.
Hoja hii si mpya. Charles Darwin aliwahi kuandika kuhusu nyigu aina ya Ichneumonidae (ichneumon wasp) ambao hutaga mayai ndani ya mwili wa mdudu-hai; watoto wa ichnemonidae hula mwili wa mwenyeji polepole (mdudu-hai) hadi afe. Darwin aliona ugumu wa kuoanisha ukatili huu wa kimaumbile na wazo la Mungu mwenye huruma kamili. Alisema hangeweza kushawishika kwamba Mungu mwenye rehema angeumba mfumo wa namna hiyo kwa makusudi.
Aidha, ni muhimu kufafanua msimamo wa wasioamini Mungu (atheists). Wengi wao hawadai kutokuamini kwa sababu tu “hawamwelewi Mungu anayefanya kazi beyond human comprehension.” Badala yake, wanadai kutumia njia zilezile zinazotumiwa na waumini wanapojaribu kumuelewa Mung, kuuliza maswali, kuchambua maandiko, kutafakari hoja za kifalsafa, na kutafuta ushahidi.
Wanapouliza maswali magumu ambayo kwa karne nyingi hayajapatiwa majibu yanayokubalika kwa wote, kuhusu uovu wa asili, na wanapoomba uthibitisho wa uwepo wa Mungu kama Allah, Mungu wa Utatu (Trinitarian God), au Yahweh, lakini hawapati ushahidi wa kimajaribio au wa kimantiki unaowaridhisha, wao huchagua kutokuamini.
Kwao, tatizo si kukataa kitu wanachokielewa; bali ni kutokushawishika na hoja au ushahidi uliopo. Kwa mantiki yao, kama madai ni makubwa, Mungu mwenye uwezo wote, mwenye kujua yote, na mwenye upendo kamili, basi kiwango cha uthibitisho kinapaswa kuwa kikubwa sawasawa na madai hayo.
Hivyo basi, swali la msingi linabaki:
Je, tatizo liko katika mipaka ya uelewa wa kibinadamu, au kuna mvutano wa kimsingi kati ya dhana ya Mungu mwenye upendo mkamilifu na uhalisia wa mateso makubwa yasiyochaguliwa na binadamu?
nothing makes sense to me.The Bible does not teach that people will float somewhere in the sky forever; instead, it says God will renew creation and live with humanity in a restored world where there is no death, pain, or evil. After death believers are with Christ, but the final promise is resurrection and a “new heaven and new earth,” meaning life forever with God in a perfected reality, not escape from creation but its complete restoration
Hamuishi kupinga uwepo wa Mungu/miungu tu bali hata supernatural phenomena.Leta huo uzaidi wa hivyo hapa.
Wewe sio Atheist, halafu unajifanya kuwajua Atheists zaidi.
Unaona hivyo?Kama ni hivi kiberiti ni uonevu wa wazi
Nimekuwekea logic hapo juu kuonyesha contradictions zilizopo kati ya The four Omnis of God and the Problem of Evil
(Epicurean paradox). Hujasoma na kuelewa.
Sasa unasema nina ego. Umetoka kujadili hoja. Umeanza kumjadili Infropreneur .
Hapa tayari umeanza kufanya logical fallacy ya ad hominem fallacy.
Badala ya kujadili hoja iliyopo mezani, unamjadili mleta hoja.
Ad hominem fallacy is a logical error where someone attacks the character, motive, or attributes of the person making an argument rather than addressing the substance of the argument itself.
It is a fallacy of relevance that attempts to invalidate a claim by discrediting the speaker.
Imenibidi nicheke unajibu vitu kaama AI, una act non human kabisa😆 sasa huyo si ni scammer jamani🤭This kind of fallacy is called red herring fallacy.
A red herring fallacy is a diversionary tactic used to shift attention away from the core issue by introducing irrelevant or off-topic information.
The goal is to mislead the audience or avoid answering a difficult question by steering the conversation toward a different, often easier-to-defend topic.
Wewe mocoservices umeleta vitu irrelevant kabisa vilivyo nje ya mada na wala havihusiani kivyovyote vile na hii mada.
Red herring fallacy.
Wewe unaelewa vp huo msemo wa Mungu wa kweli?Wakikuuliza sasahivi huyo Mungu wa kweli ni yupi atawatajia nani?
Wapo wengi , so katika uhalisia lazima kutakua yupo aliyesahihi au sivyo?Wewe unaelewa vp huo msemo wa Mungu wa kweli?
Kwa mujibu wa ulichoandika wewe pale, yeahUnaona hivyo?
Swali lako Inategemea na asili ya kitu chenyewe na aina ya uthibitisho wenye kukusudiwa.Tutajuaje kwamba hiki hakipo kwasababu ni kweli hakipo au kipo ila umekosekana tu uthibitisho wa ku prove kipo?
Kwani we unaelewa fikra huru ni nini? Ni kupinga maandiko yaliyo kwenye vitabu ama vp?Dini zishakamilika hizo mkuu, fikra huru sjajua we unapozitoa alafu bado upo humohumo
Suala hapa ni Mungu si kitu kingine.Swali lako Inategemea na asili ya kitu chenyewe na aina ya uthibitisho wenye kukusudiwa.
Ai inatambua uwepo wa Mungu ww nani upingeSuala hapa ni Mungu si kitu kingine.
Tutajuaje kwamba Mungu hayupo kwa sababu ni kweli hayupo, au Mungu yupo ila tu, umekosekana uthibitisho waku prove kwamba yupo?