Haya mambo yakuwa replaced uwa ni maneno ya kipuuzi tu.
Hivi wewe kama unamkubali msanii flani ana anatoa hits, unaweza eti shawishiwa umkubali mwingine na mtu?
Billnas alipoanza kutoka alihit kwa uwezo wake tu na kila mtu akamwelewa na chafu pozi yake. Mkmi billnas nilimwelewa sana na kuanza kumfuatilia ule wimbo alipmshirikisha TID na mpaka leo nauelewa.
Kila mwanamziki ana muda wa kuhit na kuisha, so kama una hit jiandae na maisha ya ku go down usije kufa kwa stress.
Muda ukipita umepita. Ndio maana uwa nacheka wanaosema wasanii wa zamani wanabaniwa, hakuna cha kubaniwa muda wao umepita. Ni sawa uwambie watoto wa juzi kuwa Mr nice alikuwa msanii mkubwa akipita nyomi linamfuata, uwa hafi nikirudi kusikiliza nyimbo zake nashangaa hata alikuwa anaimba nini.
Nikirudi kusikiliza nyimbo za Suma G nagundua ile michano na style haiwezi penya kwa kizazi hiki, same kwa juma nature.
Godzilla alikuwa anahisi anaishi US unyama mwingi na mziki baadae ukaanza mkataa akaanza jitengenezea mwenyewe nyimbo kwenye studio yake. Hits zake nyingi kazitengeneza Marco Chali, sijui aliamua jutegemea au waligombana hilo sijui.
Na ukumbuke kuwa waliomuibua Godzilla ni hao hao Mawingu nakumbuka kwenye hayo mashindano ya freestyle nadhani Dj fety ndie aliyekutana nao wakati akitafuta washindani. japo hakuwa mshindi wa kwanza lakini baada ya kuwa na Marco alipeea airtime kuliko hata Niki Mbishi.