Mrema David
Member
- Jul 19, 2022
- 5
- 3
Kwa miaka mingi kumekuwa na hali duni katika sekta ya michezo nchini na hii ikijumuisha michezo yote ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, mchezo wa ngumi, michezo ya madola, na kadhalika. Hali hii imekuwa ikipelekea maswali mengi kutoka kwa wadau wa michezo juu ya uwezo wa utendaji katika mamlaka zinazohusika na michezo, uwezo wa timu zetu na wanamichezo wetu kwa ujumla, pamoja na uwekezaji katika sekta hii nyeti. Katika kuhakikisha mapinduzi ya kimichezo nchini, serikali, wadau mbalimbali wa michezo na wanamichezo wenyewe wamejaribu kutafuta suluhisho, na hivi karibuni tumeanza kuona mabadiliko kuanzia kwenye mchezo wa soka. Mabadiliko haya yamekuja vipi?
Ukiangalia katika nchi za wenzetu ambazo zimeendelea kimichezo, utagundua siri moja kubwa ya maendeleo hayo ni uwekezaji mkubwa walioufanya katika michezo. Ukiachilia mbali bajeti inayotengwa na serikali kwa ajili ya mchezo katika mwaka, wadau mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wamekuwa wakiwekeza sana katika timu za michezo mbalimbali katika nchi hizo. Angalia timu za soka zenye mafanikio makubwa hapa Afrika mfano Al-Ahly ya Misri, Wydad AC na Raja Casablanca za Morocco, Esperance de Tunis ya Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini, n.k, kuna uwekezaji mkubwa sana katika timu hizi ambao unazipa nguvu kubwa sana kuanzia kwenye soko la wachezaji na kwenye mashindano kwa ujumla. Lakini pia kuna timu kama Manchester city ya Uingereza, ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Sheikh Mansour bin Zayed kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu.
Jambo lingine nililoliona kwa wenzetu ni mipango endelevu. Hii inajumuisha mfumo wa kutafuta vipaji, kuvitunza, na kuviandaa kwa manufaa ya baadae. Wenzetu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji kuanzia ngazi ya utotoni na kuvitumia kwa maendelea binafsi, jamii na Taifa kwa ujumla. Niliona wiki mbili zilizopita timu ya Chelsea ya watoto wenye umri chini ya miaka 11 ilitwaa ubingwa wa ligi ya watoto nchini Uingereza, nikajiuliza je sisi tuna mfumo kama huo? Maana watoto hawa (timu za akademi) ndio baadae wanakuja kutengeneza timu za wakubwa kwa ngazi ya klabu na Taifa na kushindana vema katika mashindano mbalimbali.
Lakini baada ya kuona hayo na mengine mengi, ninafurahi kuona miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko katika sekta ya michezo nchini. Tukibaki katika mchezo wa kandanda, tumeshuhudia wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa, watu maarufu, na wanasiasa wakiwekeza katika klabu za mpira wa miguu. Mifano hai ni Mohamed Dewji (Mo) kwa Simba, Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa Yanga, Yusuph Bakhresa kwa Azam fc, Bin Slum kwa Coastal Union, na hivi karibuni tumeona mmiliki wa Fountain Gate akiinunua Singida Big Stars ambayo kwa sasa itaitwa Singida Fountain Gate. Pia tumeona uwekezaji katika utengenezaji wa jezi na vifaa vya michezo, mfano Fred Ngajiro (Vunjabei) kwa Simba na Sheria Ngowi kwa Yanga. Tumeona uwekezaji huu umeleta mabadiliko makubwa kwa timu zetu katika ligi za ndani pamoja na ushindani katika mashindano ya kimataifa, na ni hatua muhimu katika kukuza soka letu.
Kwenye eneo la mipango endelevu na kukuza vipaji, tumekuwa na mashindano ya soka ya copa cocacola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17. Kipindi fulani tulipata timu ambayo ilienda Brazil na kufanya vizuri sana. Tulikuwa na timu nzuri sana za Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti boys) na wale wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro heroes). Najiuliza, sasa hivi tunakwama wapi? Vijana wengi wanapotea kisoka. Pengine hakuna mifumo mizuri na imara ya kuwafuatilia, kuwatunza, na kuwaandaa kwa manufaa ya baadae. Sasa hivi ligi kuu kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 inaendelea. Hii ni hatua nzuri kwa kutengeneza tena timu imara ya vijana, kuwaweka pamoja, na kuwawekea programu ya kuwaandaa kuitumikia timu ya Taifa ya wakubwa. Tuweke jicho pia kwenye michezo mashuleni, mfano UMITASHUMTA na UMISETA, kuna vipaji vingi ambavyo ni hazina kwa Taifa. Hatujachelewa, bado tupo ndani ya wakati, tunaweza kuanzia hapa na kuendelea.
Jambo lingine lililochochea mapinduzi ya soka, ni mchakato wa mabadiliko ya mifumo ya kiutendaji ndani ya klabu zetu. Miaka ya karibuni tumeshuhudia Simba na Yanga wakipita katika michakato hiyo. Moja kati ya mabadiliko hayo ni katika eneo la uongozi ambapo Simba kuna Rais wa heshima, bodi ya wakurugenzi, pamoja na viongozi wengine chini yao huku Yanga wakiwa na Rais pamoja na viongozi wengine. Katika eneo la utendaji timu hizi pia zimekuwa na nafasi za watendaji wakuu wa klabu. Eneo la ufundi pia limeboreshwa haswa baada ya timu hizi kuingia mikataba ya urafiki na baadhi ya timu za nje, mfano Al-Ahly, Sevilla, na ligi kuu ya Hispania (La liga). Sasa hivi ukiangalia mabenchi ya ufundi ya timu hizi ukiachana na walimu pamoja na makocha wa nafasi mbalimbali, utaona kuna wataalam wameongezeka, mfano wataalam wa utimamu wa mwili pamoja na timu za skauti ya wachezaji. Mbali na hayo, timu zetu pia zina idara mbalimbali mfano tumeona timu nyingi zikifanya vizuri katika eneo la matangazo na idara za habari zikisimamiwa na wasemaji wa klabu.
GOLI LA MAMA! Mwaka huu serikali yetu kupitia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilianzisha kampeni ya GOLI LA MAMA, ambapo Rais alitangaza kutoa kiasi cha 5,000,000/= kwa kila goli litakalofungwa na timu za Simba na Yanga katika mashindano ya vilabu Afrika. Kampeni hii ilileta motisha kubwa na kuifanya Simba kufika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika na Yanga kufika fainali ya kombe la shirikisho Afrika. Motisha hii imeendelea kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ambapo Rais ameahidi kutoa kiasi cha 10,000,000/= kwa kila goli litakalofungwa katika kuwania tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika.
AHSANTE GOLI LA MAMA! Nampongeza Mheshimiwa Rais pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa, na Michezo kwa kuzipa nguvu timu zetu. Ni matumaini yangu kwamba huu ni mwanzo tu, na tutaendelea tulipoishia.
Hali kadhalika tusisahau na michezo mingine pia. Mchakato huu uendelee kwa wanamichezo wetu wa mpira wa kikapu, mpira wa mikono, masumbwi, riadha, n.k. Tuwekeze, tuweke mipango endelevu, tukubali mabadiliko kimfumo na kiutendaji, pia serikali na wadau wengine tuweke nguvu ili kuhakikisha sekta nzima ya michezo kwa ujumla wake inazidi kukua na kuleta tija kwa Taifa.
Kwa pamoja tunaweza. Kazi iendelee!

Attachments
-
Alphonce Simbu London marathon 2017 (chanzo-google).jpg309.3 KB · Views: 3 -
Copa cocacola 2013 (chanzo-google).jpg134.8 KB · Views: 2 -
Goli la mama-Simba (chanzo-ukurasa wa instagram wa Simba SC.jpg188.7 KB · Views: 4 -
Goli la mama-Taifa Stars (chanzo-ukurasa wa instagram wa Taifa Stars.jpg114.1 KB · Views: 4 -
Goli la mama-Yanga (chanzo-ukurasa wa instagram wa Ndugu Gerson Msigwa.jpg167.1 KB · Views: 5 -
Hasheem Thabeet (chanzo-google).jpg80 KB · Views: 5 -
Hassan Mwakinyo (chanzo-google).jpg140.9 KB · Views: 3 -
Mabosi wa Yanga,Azam na Simba (chanzo-google).jpg21.1 KB · Views: 2 -
Mama Samia na watendaji wa Wizara ya sanaa,utamaduni na michezo (chanzo-ukurasa wa instagram w...jpg99.4 KB · Views: 3 -
Mkataba Yanga na Sevilla (chanzo-google).jpg43.6 KB · Views: 3 -
Simba vs Sevilla (chanzo-google).jpg67 KB · Views: 3 -
Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Sanaa,utamaduni na michezo (chanzo-ukurasa wa instagram wa...jpg67.1 KB · Views: 3
Upvote
1