Goli la Peter Tino lawanyamazisha wazambia, Kenneth Kaunda kwenye uwanja wa ndola, Zambia,1980

Joined
Dec 13, 2018
Posts
30
Reaction score
140
GOLI LA PETER TINO LAWANYAMAZISHA WAZAMBIA, KENNETH KAUNDA KWENYE UWANJA WA NDOLA, ZAMBIA,1980.

Leo 13:15pm,22/03/2019.

Enzi hizo nilipata kuwashuhudia Gabriel Peter (Gebo Peter) na Emmanuel Peter (Ema Peter) walipokuwa Manyema (west ham) huku Gebo huku Ema,kwenye ligi daraja la tatu ilala, mtakumbuka upinzani na nungwi, wacheche ,ilikuwa shangwe na kaka yao Star Augustino Peter (Peter Tino) alikuwa anakuja kucheki ndondo, ilikuwa safi sana.

Mwaka 1993 Simba Sports Club ilikuwa na wachezaji wazuri sana akiwemo Gabriel Peter aka Gebo Peter. Alikuwa ni namba tisa mzuri sana na alitumia urefu wake kufunga magoli mengi sana. Kikosi hicho kilikuwa na kipa nambari One Tanzania, Mohamed Mwameja pamoja na Idd Pazi, Athuman Kasongo, Twaha Hamidu, Fikiri Magoso, George Masatu, Hussein Marsha, Abubakar Salum, Edward Chumila, Gebo Peter, Damian Kimti na wengineo wengi.

Nyumbani kwao Morogoro ndipo wazazi wangu pia walipo. Wakati ule nipo Shule ya msingi Bungo,walikuwa wakipita pale kuelekea Uwanja wa Veta,Jabal hila hata Kigurunyembe kuicheki Zaragoza ambayo baadae ilikuja kuwa Moro United, Gebo na Ema na Peter (Tino) walikuwa wakija nyumbani kwao,walikuwa wakija kucheki mechi za ndondo enzi hizo Uruguay na Paraguay pale Kilakala,Morogoro,nilikuwa nahakikisha napata kunawaona mastaa awa,Hao watatu walikuwa maarufu sana Kwanzaa kule kijijini Matombo na Mgeta na Morogoro kwa ujumla.

Enzi zile ilikuwa safi sana kuona watu unaowasikia redioni. Mara ya mwisho niliwaona katika msiba wa babu yao Mzee Aloyce; ni miaka mingi sana. Peter Tino, Gebo Peter pamoja na mdogo wao Ema Peter walichangia kwa kiasi kikubwa kuiweka Morogoro kwenye ramani ya soka kama mtaikumbuka Reli Kiboko ya vigogo ambapo Reli alikuwa hafungwi na Simba wala Yanga katika Uwanja wa Jamhuri pale Morogoro, Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi! Gebo Peter,lakini bado tunao Kaka yetu, Baba yetu Peter Tino na Ema Peter kupata nasaha zao mbalimbali kuipeleka mbele Taifa Stars.

-Familia iliyobarikiwa kisoka Tanzania.

Peter Tino ndiye aliyetupeleka watanzania kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika,Lagos,Nigeria kwa mara ya kwanza,1980.

- Je ilikuwaje hapo Uwanjani Ndola.

Nakumbuka bao la kusawazisha lilitokana na Zambia kupata mpira wa kona na hivyo wachezaji wote walikwenda golini kwa Taifa Stars kutaka kufunga kona hiyo na kuacha mabeki wawili tu ambao walikuwa wanamlinda Mshambuliaji Peter Tino.

Baada ya kona kupigwa kipa wa Taifa Stars Juma Pondamali alipiga ngumi mpira ule na kumfikia kiungo Hussein Ngulungu ambaye naye baada ya kuumiliki alipiga pasi ndefu iliyomkuta Peter Tino ambapo wakati huo alikuwa amebaki na mabeki wawili tu.

Peter Tino aliukokota mpira mabeki hao wawili wakawa wanarudi nyuma Peter Tino anawafuata na mpira na ndipo alipompiga chenga beki mmoja na kubaki na mmoja ambaye alimpiga chenga na kumzidi mbio na alipofika mita 18 toka golini aliachia shuti kali lililomshinda kipa Efford Chabala na mpira kutinga wavuni na kuwa njia nyeupe kuelekea kombe la Mataifa ya Afrika, lililokuwa linafanyika jijini, Lagos, Nigeria.

Baada ya Peter Tino kusawazisha bao hilo uwanja mzima ulinyamaza na kuwa kimya kabisa isipokuwa kwa Watanzania wachache waliokuwepo uwanjani hapo ambao walikuwa wanashangilia.

-Gebo Peter na Ema Peter.

Nakumbuka sana Gebo Peter alikuwa mrefu sana mithiri ya Peter Crouch au Mwaikimba miguu ya tege kidogo kama alivyo Kaka yake Peter Tino,Alikuwa ni Super Sub wa Simba mwaka 1991 Ligi Daraja la kwanza (ligi kuu ya sasa).Naikumbuka mechi kati ya Biashara Shinyanga na Simba Sports Club, Uwanja wa kambarage Shinyanga hadi dakika ya 87 biashara 1 Simba 1, akaingia Gebo Peter na Simba wakapata mpira wa adhabu upande wa pembeni karibu kabisa na benchi la akiba la Biashara, mpigaji alikuwa Star mwingine Zamoyoni Mogella basi wachezaji wa timu zote wakajazana golini ikiwa Simba wanataka kufunga na Biashara kuokoa wapate sare (kumbuka mechi ya awali uwanja wa Taifa simba alifungwa 1-0) , Sasa Urefu wa Gebo Peter uliwazidi wachezaji wote na Zamoyoni Mogella alichofanya ni kumuita Gebo kwa nguvu sababu alikuwa ndio threat kwa Biashara basi mabeki na Kipa wa Biashara (Dhikiri Nchumila) na wachezaji wote wa Biashara wakakimbilia kwa Gebo, Mogella akapiga chop moja kwa moja likaingia wavuni, goli na mpira ukaisha..ha ha Zamoyoni Mogella aliendelea kushangilia kwa kuita Geboooooooo.Kwa hakika Augustine, Gabriel na Ema Peter ni wana familia waliobarikiwa kisoka.

-Kujituma kwa Wachezaji wa Zamani na wa Sasa.

-Wachezaji wa zamani enzi za akina Peter Tino,walicheza mpira kwa mapenzi na kwa kujituma mno kulinganisha na wachezaji wa sasa japokuwa wakati huo walikuwa hawapati fedha nyingi kama wanazopata wachezaji wa hivi sasa.

Enzi hizo kabla ya kuanza kwa mazoezi kwanza walikuwa wanafanya mazoezi binafsi kabla ya kocha hajafika na akifika wanaanza upya kwa kufuata programu ya siku hiyo aliyopanga.

Peter Tino scored a last minutes goal and made It to our Football History With Respect to AFCON ,
Who Is Next ?

-Nani kuvunja rekodi ya Peter Tino.

Je ni Mbwana Samatta!? Ama ni Simon Msuva, Je ni Shiza Kichuya ama Jonas Mkude!?
Ni muda sasa wa kuvunja historia ya Straika wa zamani wa Pan Afrika, Peter Tino, aliyepiga krosi ya dhahabu kuwafunga Wazambia pale Lusaka, mchana wa siku ya Jumamosi na kutupeleka katika michuano ya Mataifa ya Afrika,mwaka 1980.

Kuelekea mchezo wa Tanzania na Uganda,Tutakwenda kumuenzi Shujaa Peter Tino, Mluguru wa Matombo,Morogoro,Kaka yetu,Baba yetu aliyefanya jitihada kwa ufundi mkubwa akafunga Goli kule Lusaka, Zambia lililotupeleka Lagos, Nigeria kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza na sisemi ya mwisho 1980 japo
rekodi imesimama hadi leo. .

Ili kumuenzi Peter Tino na kuwapa hamasa Watanzania na Wachezaji Kuelekea mechi na Uganda siku ya jumapili
nashauri barabara ya Vingunguti Kiembe Mbuzi alipokuwa anakaa Shujaa Peter Tino,ufanyike utaratibu na mtaa uitwe "PETER TINO STREET " ama

"PETER TINO ROAD " hii ndio njia pekee ya kumuenzi shujaa Peter Tino aliyetupeleka Afcon kwa mara ya kwanza mwaka 1980 na haijatokea tena.Itakuwa ni kumbukumbu nzuri na heshima kwake na wanamichezo wote kufanya matukio ya kirekodi kitaifa na kimataifa
Naamini Waziri Wa Michezo au Mkuu wa Mkoa kwa nafasi yake anaweza kufanikisha hili,
Mungu Ibariki Taifa Stars tuweze kuingia tena kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya pili, siku ya jumapili, kesho kutwa.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Usinikumbushe hii combination Mkuu: Mohamed Mwameja pamoja na Idd Pazi, Athuman Kasongo, Twaha Hamidu, Fikiri Magoso, George Masatu, Hussein Marsha, Abubakar Salum, Edward Chumila, Gebo Peter, Damian Kimti.

Wako wapi hawa watu? Dah! Ilikuwa balaa hii!
 
Aiseee andiko swadakta kabisa!

Kusema kweli Peter Tino anastahili kuenziwa,ikizingatiwa ilivyokuwa vigumu kupata ushindi dhidi ya KK eleven pale Ndola.Maana ile KK 11 ya akina Moses Chikwarakwara ilikuwa moto kweli kweli.
 
Edward Chumila (Marehemu)
 
Ile ndio Taifa Stars bhana haikumuhitaji le mutuz na Wema ili ishinde.

Wachezaji walikuwa na uzalendo uliopitiliza ukizingatia walikuwa wachezaji wa ridhaa!

Kila la kheri Mbwana Samatta!
... sana Kiongozi. By then Wema alikuwa vidudu au hajazaliwa na wengine walikuwa maporini huko Dar wanaisikiaga tu. Kama magwiji wenyewe wapo, kwanini wasitumiwe kuleta hamasa? Inakera sana!
 
Yani kwa kifupi,wanachofanya leo akina zidane,,ronadinyo,,cr7,,JJ okocha,,

ndo walivyokua wanafanya akina gebo,pitatino,,Hussein masha,khamis gaga,makumbi juma,,n,k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ramadhan Lenny,,,,,lakini Mimi siyo mkia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…